Air Tanzania among entities that borrowed money without approval, says PAC


Mkuu una moyo kweli kuwasemea hawa wanunuzi wa ndege. Btw ATCL ilifufuliwa au imefufuliwa? Tunaongea shirika la umma kufufuliwa - as a going concern in its real sense.
 

Kaka! Wewe ni muumini wa collective responsibility na umeisema sana humu. Ni bahati mbaya kuwa JPM hawezi kuchomoka humu kama serikali inanunua ndege na kuzikabidhi kwa ATCL huku pia akiteua mkurugenzi mkuu wa ATCL ili aiendeshe!! Iwe ni katika manunuzi au matumizi, mwisho wa siku ni pesa imepigwa!!

Kwa dhana ya collective responsibility, serikali ndio ikiyochukua jukumu la kufufua ATCL. Haiwezi kujitoa katika lawama na hasa kama ilihamishiwa kwenye kundi la mashirika yasiyochunguzwa na CAG kipindi cha yule profesa!
 
Very sad as the flights travelling abroad run the risk of being impounded because of the huge debts and the related interests.
 
Mkuu Jay One inaonekana unamjua vilivyo Matindi. Weka CV yake hapa tukusaidie kudadavua kama anafaa au hapana
 
P.msimamizi wa serikali ni bunge au ni nani na kamani bunge hilo bunge limetokana na chama gani.ni kweli serikali ni mtekelezaji lkn hiyo serikali imeundwa na nani?
Mkuu katitu, ndio maana nimesema somo la elimu ya uraia, inahitajika sana kwa wengi wetu, hawawezi kutofautisha chama, serikali na Bunge, hata ikiwa CCM ndio chama tawala, hivyo ni serikali ya CCM, na Bunge ni Bunge la CCM, lakini bado serikali sio CCM wala Bunge sio CCM. Chama ni mpangaji tuu, serikali ni mtekelezaji, Bunge ni msimamizi, kitu ambacho ni tatizo, ni kitu kinachoitwa "the principle of separation of powers, checks and balance". Serikali inaundwa kwa mihimili mitatu, Serikali, Bunge na Mahakama, kwenye mihimili yote hakuna mambo ya uchama, Chama kinatumika tuu kupata uwakilishi na kushinda uchaguzi kwa kutumia ilani yake. Kiongozi akiisha chaguliwa, hawi tena kiongozi wa hicho chama, anakuwa ni kiuongozi wa umma, hivyo rais wa JMT, wabunge, madiwani, sio rais wa CCM au wabunge sio wabunge wa CCM etc, hivyo hoja kuwa CCM imefanya hiki au kile ni hoja muflis. Mimi kosa langu kubwa humu siku zote kuusema ukweli mchungu, watu wasiopenda kuusikia!. Tanzania bado hatuna any serious opposition ya kuiondoa CCM madarakani, hivyo ninapowaambia wapinzani makosa yao, hawaamini, anayewakosesha wapinzani kuingia ikulu, pamoja na mambo mengine, ni ujinga wa kuamini kuwa adui yao mkubwa ni CCM ndiye anayewakosesha Ikulu, nakutolea mfano mzuri kabisa, wa numbers don't lie.
Ule uchaguzi wa 2010, CCM ilijinasibu ina wanachama milioni 3. Tanzania ina watu milioni 55, watu wenye sifa za kupiga kura ni watu milioni 35, lakini watu waliojiandikisha kupiga kura ni watu milioni 20 tuu. Mtu mwenye akili lazima ajiulize hawa watu milioni 15 ambao hawakujiandikisha kwa nini?. Ukosefu wa elimu ya uraia. Kati ya hao milioni 20, miongoni mwao ni wale milioni 3 wa CCM. Siku ya kupiga kura, watu waliojitokeza kupiga kura ni watu milioni 8 tuu, hii maana yake wale watu milioni 3 wa CCM ni miongoni mwao. Matokeo ya uchaguzi, ni JK akachaguliwa kwa kura milioni 5!. Kati ya hizo, ni zile kura milioni 3 zao, na kura milioni 2 za Watanzania wengine. Mtu yoyote serious, atajiuliza kwanini watu milioni 12 wamejiandikisha, lakini hawakujitokeza kupiga kura?.

Toka 2015-2020, nimekuwa nikitoa elimu ya uraia bure humu JF, nikawashauri opposition, msihangaike na hao milioni 3 wa CCM, watafuteni wale milioni 15 ambao hawakujiandikisha, na wale milioni 12 waliojiandikisha, lakini hawakujitokeza.

CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni

https://www.jamiiforums.com/threads...get-adui-mkubwa-sio-ccm-bali-ni.310532/page-7
P.
 

Pesa imepigwa kwenye manunuzi ,yaani ni DJ(Dotto James) na JIWE ndio walikuwa wanunuzi wakuu ,hakuna kupitia bungeni wala hazina halafu cash ili kila mtu afe na chake.
 
Lengo la atcl ilikuwa kuleta watalii wengi nchi Iingize kipato je imefanikiwa? Maana kila siku tunaona watalii wakishushwa Kia na Zanzibar na Ndege za wazungu ! Ushauri bora Ndege zote ziuzwe ela iende Kwenye miradi ya maendeleo kama barabara , reli , bandari, hospitali, umeme, maji nk

Ttcl nayo iuzwe yote.

Billioni 896 ni ela nyingi hizo ukichanganya na Bei za ndege zote kama trilioni 2.3 hizo ela zinatosha kumalizia vipande vilivyobaki vya sgr Dar to Mwanza .
 
wizi , utapeli , umalaya na ujambazi ulipungua kwa kuwa watu walikuwa busy kuzalisha ila kwa sasa tutaipata fresh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…