Air Tanzania fanyeni marekebisho ya ndege zenu

Air Tanzania fanyeni marekebisho ya ndege zenu

Mkuu acha ajuaji usio na maana kitu kikikushindi omba msaada kwa wahusika ndege mpya ina mwezi mmoja tu unaleta ujuaji wako hapa ili tujue na wewe ulienda china.
 
Tarehe 30-12-2023 nimepanda ndege yenu iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou iliyopewa ruti namba TC 402.
Button za viti ambazo utumika kuweka kiti kwa mkao anaoutaka mtumiaji nyingi zimeharibika.Hili linapelekea msafiri kutokuwa na uwezo wa kuweka kiti atakavyo na kupelekea kero kubwa kwa wasafiri waliopewa siti ambazo hizo button ni mbovu.
Vyoo vinatoa harufu,nunueni pafyumu za kupulizia kwenye vyoo vya ndege.
Nawashauri fungueni ukurasa hapa JF hili tuweze kuwa na fursa ya kuwashauri kwa minajili ya kuboresha huduma ya shirika letu.
Nadhani suala la choo ni jukumu la mzabuni wa huduma za ndege ambaye kwa ATCL lazima atakuwa ni ndugu wa mkubwa wa shirika au hata ndugu wa kiongozi huko juu serikalini hivyo kumkemea mzabuni huyu kunaweza kugharimu ajira ya mkemeaji.

Zaidi, hiyo route ATCL ndiyo ina ukiritimba nayo kwenda na kurudi Dar, tabia ya ukiritimba ni kwamba kwa kuwa hakuna ushindani basi unafanya kazi chini ya kiwango kwa faida kubwa.

Hii ndiyo hali inayojiri TANESCO, TPA, TRC, DAWASA na sasa tunaenda pia kushuhudia hiyo hali PSSSF baada ya merger.
 
Back
Top Bottom