Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Hapana, ATCL ni shirika, serikali haifanyi biashara ATCL Inaweza kufa lakini si serikali.Mkuu, ATCL ni serikali, Wakala ni serikali. Ndege ni za serikali.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana, ATCL ni shirika, serikali haifanyi biashara ATCL Inaweza kufa lakini si serikali.Mkuu, ATCL ni serikali, Wakala ni serikali. Ndege ni za serikali.
Nadhani huelewi maana ya serikali haifanyi biashara. Unasema ATCL ni shirika, sio shirika la serikali?Hapana, ATCL ni shirika, serikali haifanyi biashara ATCL Inaweza kufa lakini si serikali.
Unajua, kila unaposoma post za mtu ni rahisi sana kuona nani hakupata nafasi ya kupata elimu ya juu. Ni wazi wewe ni mmojawapo. Tutajitahidi kuongeza nafasi za elimu ya juu nchini, ila nachokushauri kwa sasa ni kwamba jikite zaidi kwenye Forum za Udaku na Ucheshi, huku waachie watu waliopata nafasi za elimu ya juu.Mbona unapanic pimbi wewe! Yaan unafurahia mandege mengi ambayo mpaka yanakosa abiria inabidi yaote jua pale jnia? Unanunua ndege after 2 months unapeleka service ya billion kadhaa zaidi ya ulichoingiza, af unashangilia ugolo? Acha unafiki na usijilinganishe na Kenya chief kwa lolote. We subiri MTU aote akuleeteeni kama sheria mfate.
Hapana ndege ni za wakala wa serikali sio za serikaliMkuu, ATCL ni serikali, Wakala ni serikali. Ndege ni za serikali.
Unajua, kila unaposoma post za mtu ni rahisi sana kuona nani hakupata nafasi ya kupata elimu ya juu. Ni wazi wewe ni mmojawapo. Tutajitahidi kuongeza nafasi za elimu ya juu nchini, ila nachokushauri kwa sasa ni kwamba jikite zaidi kwenye Forum za Udaku na Ucheshi, huku waachie watu waliopata nafasi za elimu ya juu.
Usipopitia elimu za juu ni vigumu sana kujua upi ni ujinga na ipi ni busara katika mambo haya. Hivyo nakuelewa.Hakika njaa c kitu kizuri. Endelea kusifia ujinga
Shamba la mirungi la msomali na mbuzi ni wa msomaliMkuu, ATCL ni serikali, Wakala ni serikali. Ndege ni za serikali.
Kweni mkuu ATCL linapata faida kiasi gani?Mleta uzi kasema ukweli mtupu ambao watu wengi kutoka pinga pinga fc hawapendi kuusikia,
Kenya airways wanamiliki ndege 3 tu na ni shirika linalojiendesha kwa hasara miaka na miaka,
Msipende sana story za vijiweni muwe mnatembelea lile jukwaa lao kule muone namna tunavyo waumbua Maana watu wengi mumekaririshwa sana ujinga, njooni kule tuwafumbue 😂😂😂
Atcl imefufuliwa lini?Kweni mkuu ATCL linapata faida kiasi gani?
Sijui mkuu ni lini ilifufuliwa maana hata kipindi cha jk ilikua na ndege moja isiyofanya kazi na ilikua na wafanya kazi 100 ambao walikua wanalipwa mshahara kama kawaidaAtcl imefufuliwa lini?
😵Huwa ni mara chache naunga mkono hatua za Magufuli lakini kwa hili la kununua ndege niliona kwamba ni mkakati ambao unaweza kuwa na manufaa kwa Tanzania. Nilikumbuka matatizo tuliyopata baada ya kuingia mkataba na South African Airways ambao walitukodishia ndege zao na tukapata hasara kubwa sana. Hata hivyo bado nina mashaka sana na uendeshaji wa Air Tanzania na menejimenti yake.
Watanzania wengi sana hupenda kuilinganisha Tanzania na Kenya, na kuona kwamba wanatuzidi sana, kuanzia mambo ya elimu, ushindani nafasi za kazi, na hata umahili wa shirika la taifa la ndege.
Sasa kuna tetesi kwamba Shirika la ndege la Kenya, katika ndege zote wanazotumia wao wanamiliki ndege tatu tu, na nyingine zote sio za kwao ni za mashirika na watu binafsi, kutia ndani vigogo wa Kenya. Na inaonekana kwa sasa Kenya Airways wana hali ngumu sana kifedha kutokana na kuendesha shirika kwa kutumia ndege za kukodi. Kwa hiyo ukilinganisha Tanzania na Kenya, kwa kuwa sisi tuna ndege za Air Tanzania tisa ambazo ni zetu wenyewe, tofauti na wao wenye kumiliki ndege tatu tu, sie tuko mbali sana na kuwazidi katika suala la shirika la ndege la taifa.
Kumbuka kwamba ukikodi ndege kama shirika la ndege, unailipia hata kama haifanyi safari, au inafanya safari kwa hasara. Hali ni tofauti kama unatumia ndege zako mwenyewe, unaweza hata kuzipaki mwezi mzima, kutegemea na hali ya biashara, bila kujali sana kwa kuwa ni zako.
Hali ngumu ya Kenya Airways imefanya hata kuwe na mpango wa kulikabidhi shirika hilo viwanja vyote vya ndege nchini humo viwe mali zake. Tetesi zinasema pendekezo hilo linatokana na wanasiasa vigogo wa Kenya ambao baadhi yao wanamiliki ndege za Kenya Airways, na baada ya kuona faida kubwa inayopatikana toka viwanja vya ndege, njia pekee ya kufaidika na faida hiyo ni kuvifanya viwanja hivyo vimilikiwe na Kenya Airways ambako wana shares. Wadau wazalendo wa Kenya wanapinga hatua hiyo, kwamba haileti maana kukabidhi viwanja vya ndege toka kampuni ya taifa ya Kenya Airport Authority (KAA) inayofanya kazi vizuri na kwa faida na kuviweka nchini ya Kenya Airways (KQ) ambao wanapata hasara kila mwaka. Hiyo ndiyo Kenya ya wenzetu.
Update on thread: Sio tetesi tena, source ni Daily Post ikiripoti jambo lililojadiliwa na Kamati ya Bunge
DAILY POST: SHOCK as it emerges KQ owns 3 planes only, 25 planes are owned by corrupt businessmen and State operatives - KINOTI please
View attachment 1037779
View attachment 1037780