Bonheur Travels Tanzania
JF-Expert Member
- Dec 29, 2020
- 252
- 499
Tumeanza kutoa huduma ya kusafirisha abiria wanaotumia ndege kusafiri, iwe ni ndani ya nchi au kimataifa, kwa miaka kadhaa sasa. Uzoefu tulionao umepelekea tuzifahamu changamoto nyingi kupitia feedback tunazozipata kutoka kwa wateja/abiria.Miongoni mwa changamoto hizo tumejaribu kuzitolea elimu na ufafanuzi kwenye threads zetu zilizopita. Leo tumeona tugusie changamoto ya bei ya nauli.
Bei za Tiketi za #AirTanzania zimekuwa zikilalamikiwa na kufanya usafiri wa anga kuwa anasa badala ya huduma. Ni mara nyingi mno tumelazimika kutumia nguvu ya ziada kushawishi wateja kuona kwamba gharama hizi zinaendana na viwango vya huduma nzuri zitolewazo na ATC. Pia tunatumia kete ya kuwasihi watanzania kutanguliza uzalendo kwani Shirika hili bado linajipanga kibiashara, lakini inafikia hatua tunaishiwa sera!
Baadhi ya threads hapa JF ambazo zimeongelea gharama za ndege za ATCL kuwa sio rafiki na hazivumiliki ni pamoja na;
Watumiaji wa usafiri wa ndege tunajuta kwanini Serikali imenunua ndege zake
Kabla ya Mwaka 2015. Tanzania ilikuwa na mashirika ya ndege za ndani Makubwa manne. 1. Air Tanzania 2. Community air line 3. precision air. 4. Fast jet. Community air line ilirudi kwa kishindo mwaka 2008. Ililet ushindani mkubwa katika soko la ndege. Mpaka sisi Manyonge ( makapuku) tukaweza...
ATCL bado sana kwenye Safari za anga
Rais JPM anajitahidi kufufua shirika letu la ndege lakini namna linavyojiendesha ni tatizo. Tusipopiga kelele litakufa tena na juhudi za kulifufua zitakuwa zimehujumiwa. Muhula wa masomo China umemalizika. Wanafunzi waliohitimu wanarudi makwao. Nchi nyingi zinachukua wanafunzi wake kwa ndege...
Swali la Uzalendo: What is The Magic of The Same Route? Precision Air Full Flight, ATCL Half Empty
Wanabodi, Japo hoja hii inge fit best kwenye Jukwaa la Habari Mchanganyanyiko, lakini kwa vile hii ni issue ya political economy ya uchumi wa nchi, nimeshuka nayo kwenye Jukwa la Siasa. Naomba nianze na declaration ya uzalendo, mimi ni mdau mkubwa wa Shirika letu la Ndege, ATCL, hivyo...
Kwa utafiti wetu ambao sio rasmi, tumegundua Watanzania wengi wanatamani kutumia usafiri huu lakini wanaogopa bei, hasa wale wenye kipato cha kawaida. Routes mpya za Chato na Arusha zilitia hamasa lakini bei zimewarudisha wengi wao nyuma baada ya kukutana na bei tata. Ni idadi kubwa ya watu ambayo ingeweza kulizalishia shirika faida na kurahisisha safari za masafa marefu zikiwemo za kutoka Dar kwenda Mwanza, Kagera, Kigoma n.k. na kinyume chake.
Tunafahamu, lengo la Serikali na Shirika ni kuhakikisha Ndege hizi zilizonunuliwa kwa wingi zinakuwa affordable kwa watanzania wanaofanya safari (ndani na nje ya nchi). Na sisi kwa uzoefu wetu na tabia za wateja tunaliona hili la bei kuwa kikwazo namba moja kinachosababisha hata rate ya wasafiri ku-book ndege hizi za ndani ikishuka au kushindwa kuongezeka katika kiwango kinachoridhisha.
Imefikia hatua zipo baadhi ya routes za ndani zina gharama ya juu zaidi kulinganisha na gharama za ndege kupitia mashirika mengine kwenda nje ya nchi. Hatuingilii mamlaka, tunajaribu tu kufikisha 'picha halisi' kutoka kwa watumiaji wa huduma na mtazamo wetu wadau wa sekta hii muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Ni matarajio yetu wanaofanya maamuzi wataliangalia hili kwa ukaribu na kulifanyia kazi haraka. Wakishusha bei, tutasafirisha watanzania wengi popote pale kwa kweli na ndege hazitasafiri tupu, kwani wengi wapo tayari tatizo ni hilo tu- BEI!
Au abiria wazoefu na watarajiwa mnasemaje?