Air Tanzania ingeshusha viwango vya nauli, tungesafirisha Watanzania wengi ndani na nje ya nchi

Uzi wako ungetakiwa uweke bei ya sasa toka sehemu moja kwenda nyingine alaf uje na bei ambayo wewe unaona italeta ushindani. Hapo mjadala ungekuwa poa sana.
 
Nimeshuhidia mara zaidi ya 4 ndege inatua uwanja wa Dodoma ikiwana abiria wasiozidi 4, kuna siku ilitua na abiria wanne
 
Uzi wako ungetakiwa uweke bei ya sasa toka sehemu moja kwenda nyingine alaf uje na bei ambayo wewe unaona italeta ushindani. Hapo mjadala ungekuwa poa sana

Asante kwa wazo zuri mkuu.

Tulifikiria kufanya hivyo awali, lakini tukaona tuambatanishe nyuzi ambazo zinaonyesha viwango vya bei na mapendekezo kuepuka kurejea topiki.

Asante.
 
Nimeshuhidia mara zaidi ya 4 ndege inatua uwanja wa Dodoma ikiwana abiria wasiozidi 4, kuna siku ilitua na abiria wanne
Tafakari nauli ya kutoka Dodoma kwenda Dar ni sh.276,000/= Economy na sh.322,800/= Business.
Unaweza kufika ofisini ukaelezwa kuna nafasi ya Business !
 

Upo sahihi mkuu. Bei zinazokubalika na wengi na ofa zimekuwa ni chachu kwa abiria wengi kupanga safari ukiachana na wale wa dharura. Tumekuwa tukipokea bookings nyingi baada ya wateja kuvutiwa na bei/ofa tu za safari.
 
Nimeshuhidia mara zaidi ya 4 ndege inatua uwanja wa Dodoma ikiwana abiria wasiozidi 4, kuna siku ilitua na abiria wanne
Mkuu uko sahihi. Wajifunze kwa shirika letu la Tanesco, kabla ya kuja na mpango wa makusudi wa kuongeza idadi ya wateja umeme ulikuwa ni anasa lakini baada ya kupanua wigo wa wateja wao ambapo sasa almost 80 percent of the households wana access ya umeme tumeona bei zikishuka na kuwa affordable kwa wengi. Atcl igeni hiyo itawasadia maana wengi tunatamani tupande ndege zenu kikwazo ni gharama.
 
Umeeleza vizuri sana mkuu
 
Niwe tu wazi,nitafurahi sana likifa hili lidude. Nitashangilia sana. Fastjet itarudi hewani.
 
Mkuu nyie mnahusika na mashirika yote yote ya ndege?
 
Nimeshuhidia mara zaidi ya 4 ndege inatua uwanja wa Dodoma ikiwana abiria wasiozidi 4, kuna siku ilitua na abiria wanne
Imefikia hatua hata wale wenye uwezo wa daraja la kwanza nao wameona bei ni kubwa. Nimeona wengi wao wanaikimbia wanasafiri na private car. Kuna jamaa yangu manager bank fulani dar,walikuwa na harusi mbeya mwezi wa 11,walikuwa 6,wote wanakuja kwenye hiyo harusi. Wakaniulizia gari gani ni zuri dar to mbeya?. Nikaulize hata wewe kwa nini msipande pipa? Akajibu tumeenda kuuliza bei zake hatuziwezi ni kubwa hatari. Baadae wakaamua tu kubanana kwenye Rav 4
 
Fastjet walikuwa wabunifu sana kwenye maswala ya usafiri wa anga. Wale jamaa wangeachwa wangeteka soko la usafiri kwa Tz. Walikuwa na amsha amsha za kutosha,offer offer zao zilikuwa zinawafanya hata wengine wasiosafiri waamue kusafiri kwenda tu kutembea mahala. Zilikuwa zinatamanisha/zinakuvuta usafiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…