Air Tanzania ingeshusha viwango vya nauli, tungesafirisha Watanzania wengi ndani na nje ya nchi

Kabisa mkuu. TANESCO wako vizuri sana kwa sasa. Natamani sana pia tufungue tred kwa ajili ya haya mashirika ya maji. Siku hizi maji imekuwa ni kitendawili na kama anasa kwa sasa. Nao waige mfano wa TANESCO. Wanakuchaji hata kama maji hupati. Unit zao ni gharama kubwa. Zamani umeme walikuwa juu kuliko maji kwa gharama. Lakini siku hizi maji wako juu kuliko umeme
 
Ni kweli; katika mazingira yetu inabidi Air Tanzania indeshe biashara yake kwa kuvutia sales volume kubwa kuliko kuangalia revenue per sale tu.
 
Nauli za usafiri wa anga zilishaanza kushuka naturally kutokana na free market competition.Tena bila kuharibu service sana. Ndege fulani dekta binafsi walikuwa creative kwa kiasi chao, licha ya changamoto nyingi Tanzania.

Serikali ilivyoleta kimbelembele chake kufufua ATCL bila kununua ndege kwa open tender process wala business plan ya kueleweka na kuingilia buashara ya usafiri wa anga ndiyo imepandisha nauli za usafiri wa ndege.

Mtu hana hela, hana uwezo wa kulipa nauli kubwa, unamwambia apande kwa uzalendo.

Akija kununua tiketi kwa kusema hana hela ana uzalendo, anataka kununua tiketi kwa uzalendo, atapewa hiyo tiketi?

Hii serikali inaharibu mambo yenyewe kwa kuingilia biashara bila mpango.

Tumeona hili katika biashara ya korosho. Linajirudia tena katika biashara ya usafiri kwa ndege.

Wewe hujajiuliza kwa nini vitabu vya ATCL havikukaguliwa na CAG kama ilivyo taratibu kila mwaka?

Wanaficha nini?
 
Mkuu nyie mnahusika na mashirika yote yote ya ndege?
Ndio mkuu. Sisi tunashirikiana na mashirika mbalimbali ya ndege katika kazi zetu.

Baadhi ya mashirika hayo ni ATCL, Etihad, Precision Air, KQ, Emirates, KLM, RwandAir, Fly Dubai, Turkish Airways, Qatar Airways na Egypt Air.

Karibu sana.
 
Fastjet salute kwao. Watu tuli enjoy kwa kweli, unasafiri na familia nzima dar to mza 5persons nauli hata million haiishi, hiyo ni go and return, sijui hizo enzi zitarudi kweli? Sasa Ni mwendo wa mabasi tu.
 
Zitarudi mkuu,tena safari hii ndio itarudi kwa kasi. Tuliombee tu hili lidude life na litakufa kweli,kama linabeba watu wa4 kwa trip. Nawaombea Fastjet waje na jina jipya na wajisajiri upya ili kuondokana na kufanyiwa fitina tena
 
Ndio mkuu. Sisi tunashirikiana na mashirika mbalimbali ya ndege katika kazi zetu.

Baadhi ya mashirika hayo ni ATCL, Etihad, Precision Air, KQ, Emirates, KLM, RwandAir, Fly Dubai, Turkish Airways, Qatar Airways na Egypt Air.

Karibu sana.
Sawa mkuu. Nakuomba hawa jamaa msiwashtua. Ikiwezekana muwe mnawapanga kwamba tuko uchumi wa kati watu wana hela nyingi pandisha pandisha nauli. Abiria wakisafiri wanne waambieni ni upepo tu unapita,ili ku-cover hao hao waliopo wachache ni kuwapandishia nauli hata mara 3 yake. Maana hakuna jinsi sasa
 
Hapana mkuu. Lengo letu ni kujaribu kufikisha mawazo na mtazamo wetu kama wadau katika sekta hii, ili kusaidia wasafiri ambao kimsingi ni wateja tu pia.
 
UPDATE:
Tumepokea taarifa njema (sio rasmi) kwamba maoni yanayotolewa kwenye uzi huu yanafuatiliwa kwa umakini na mamlaka husika kwa lengo la kufanya maboresho.

Hili kwetu ni jambo la kuvijunia kuwa sehemu ya kuchochea uboreshaji huduma katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya Anga.

Shukrani na pongezi zaidi ziwafikie nyote mnaoshiriki na kutoa ukosoaji wenye tija na mapendekezo.

Tuendelee kuiboresha sekta hii kwa kila mdau (hata abiria na abiria watarajiwa wote ni wadau pia) kwa nafasi yake.

Sisi Bonheur Travels Tanzania tunajikita zaidi kwenye kutoa elimu kwa umma na huduma bora kwa kadri tuwezavyo!
 
Nimekuwa nikisema siku nyingi kwamba consumer advocacy groups are as important as political parties, if not more.

Na katika vitu ambavyo havipo, au havipo active Tanzania, ni hizi groups.
 
Ndio mkuu. Sisi tunashirikiana na mashirika mbalimbali ya ndege katika kazi zetu.

Baadhi ya mashirika hayo ni ATCL, Etihad, Precision Air, KQ, Emirates, KLM, RwandAir, Fly Dubai, Turkish Airways, Qatar Airways na Egypt Air.

Karibu sana.
Washauri waweke tiketi hata za miezi mitatu mbele, nalipa january napanda march mwishoni, kama nauli ni 340000 mimi nilipe 120000, nipo nchi moja ya asia huku ndege local sio anasa
 
Nimekuwa nikisema siku nyingi kwamba consumer advocacy groups are as important as political parties, if not more.

Na katika vitu ambavyo havipo, au havipo active Tanzania, ni hizi groups.

Hakika Mkuu. Ndio maana sisi tunajaribu kujiweka nafasi hii ya kutetea consumers kwa sababu tunakutana na changamoto zao awali kabisa. Tunafanya hivi tukiamini mamlaka husika hazitachukulia tofauti.
 
Washauri waweke tiketi hata za miezi mitatu mbele, nalipa january napanda march mwishoni, kama nauli ni 340000 mimi nilipe 120000, nipo nchi moja ya asia huku ndege local sio anasa

Sawa sawa mkuu. Asante kwa maoni mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…