Air Tanzania yaanza safari Dar - Musoma, Demand ya ndege kanda ya ziwa ni kubwa sana na zinajaa

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
✈️ 17/9/2026: Air Tanzania yaanza rasmi safari za Dar es Salaam > Musoma > Mwanza > Dar

hatua hii inayoongeza muunganiko wa usafiri wa anga kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kanda ya Ziwa.

Licha ya nauli kuwa juu, uhitaji wa usafiri wa ndege Kanda ya Ziwa umeendelea kuwa mkubwa sana, ukiakisi ongezeko la mahitaji ya safari kati ya miji ya kanda hiyo na Dar es Salaam.

Kwa sasa, Mwanza, Bukoba, Mara na Geita zinaendelea kuwa sehemu muhimu katika mtandao wa safari za anga wa Kanda ya Ziwa

Uwanja wa ndege wa Shinyanga umekamilisha ujenzi, huku hatua ya uzinduzi ikiwa bado inasubiriwa. Kwa mujibu wa matarajio yaliyopo, uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Mwanza ni uwanja wa pili unavyohudumia idadi kubwa ya abiria wa ndani nchini
 
NI mapokeo tu. Kama bar mpya. Inajaa baada ya muda mfupi walevi wanarudi kwenye grocery walizozoea.
Kanda ya ziwa kwa domestic flights haina mpinzani

Kama umewahi kufika airport ya Mwanza utajua tu

Ndio uwanja wa pili nchini kwa kupokea abiria wa ndani

Kuna abiria wengi sana wa Mara walikuwa wanashukia hapo

Next >>>>> Shinyanga. Wazee wa Kahama watawakilisha vema sana.
 
Tumeambiwa hiyo ni mikoa/sehemu iliyojaa umasikini.Sasa,inakuwaje wawe na uhitaji wa usafiri wa gharama kubwa na wa Starehe?Au wanakopeshwa?
Haina relation na watu kupanda ndege, hata kama eneo lina umasikini wapo wanaoenda mikoa mingine kusoma, kuajiriwa, kufanya biashara, n.k.

pia ndani ya hio mikoa zipo fursa nyingi kuanzia madini, kilimo, biashara, n.k.

Fika Bukoba ushangae, kuna abiria wengi domestic kuzidi hata Mbeya, watu wanalalamika ndege inajaa haraka
 
"Haina relation/uhusiano"? Kivipi?Kwa hiyo wana mahela na umasikini unaotajwa ni puruzai tu?
Kumbuka kanda ya ziwa ndio eneo lenye watanzania wengi ndani ya kanda pamoja na waliosambaa kwengine.

Huko ni kawaida kukuta familia ina watu nane,

Umaskini unaotajwa ni kweli upo lakini pia wenye vipato nao wapo wengi tu,

halafu tupo nchi yenye free movement, kwenu kunaweza kuwa na umasikini ila umeenda kutafuta fursa mikoa mingine, mfano kuna watu wamesoma wameajiriwa kwenye taasisi kubwa na makampuni nje ya huko kwao, wakitaka kurudi kwao watashindwa kupanda ndege ?
 
✈️ 17/9/2026: Air Tanzania yaanza rasmi safari za Dar es Salaam > Musoma > Mwanza > Dar

hatua hii inayoongeza muunganiko wa usafiri wa anga kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kanda ya Ziwa.

Licha ya nauli kuwa juu, uhitaji wa usafiri wa ndege Kanda ya Ziwa umeendelea kuwa mkubwa sana, ukiakisi ongezeko la mahitaji ya safari kati ya miji ya kanda hiyo na Dar es Salaam.

Kwa sasa, Mwanza, Bukoba, Mara na Geita zinaendelea kuwa sehemu muhimu katika mtandao wa safari za anga wa Kanda ya Ziwa

Uwanja wa ndege wa Shinyanga umekamilisha ujenzi, huku hatua ya uzinduzi ikiwa bado inasubiriwa. Kwa mujibu wa matarajio yaliyopo, uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Mwanza ni uwanja wa pili unavyohudumia idadi kubwa ya abiria wa ndani nchini
Umeangalia Dar-Kilimanjaro (KIA), KIA- Mwanza, KIA-Zanzibar, KIA-Nairobi? Hapo bado kuna ARUSHA airport au unajifariji na Katoro?
 
KIA imepitwa na Mwanza kwa abiria wa ndani

KIA ina abiria wengi wa nje

Serengeti International Airport ikifanikiwa kujengwa, KIA itakauka sana, ni jambo la muda tu mtajua hizo airport zilijaa kwasababu ya kukosekana kwa uwanja mkubwa karibu na Serengeti
 
Dar-KIA, KIA-Zanzibar na KIA-Mwanza hao ni abiria wa nje? Ama kweli ujinga mzigo wa nnya.
 
KIA imepitwa na Mwanza kwa abiria wa ndani

KIA ina abiria wengi wa nje

Serengeti International Airport ikifanikiwa kujengwa, KIA itakauka sana, ni jambo la muda tu mtajua hizo airport zilijaa kwasababu ya kukosekana kwa uwanja mkubwa karibu na Serengeti
Huu ni ukweli mchungu sana.
 
✈️ 17/9/2026: Air Tanzania yaanza rasmi safari za Dar es Salaam > Musoma > Mwanza > Dar

hatua hii inayoongeza muunganiko wa usafiri wa anga kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kanda ya Ziwa.

Licha ya nauli kuwa juu, uhitaji wa usafiri wa ndege Kanda ya Ziwa umeendelea kuwa mkubwa sana, ukiakisi ongezeko la mahitaji ya safari kati ya miji ya kanda hiyo na Dar es Salaam.

Kwa sasa, Mwanza, Bukoba, Mara na Geita zinaendelea kuwa sehemu muhimu katika mtandao wa safari za anga wa Kanda ya Ziwa

Uwanja wa ndege wa Shinyanga umekamilisha ujenzi, huku hatua ya uzinduzi ikiwa bado inasubiriwa. Kwa mujibu wa matarajio yaliyopo, uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Mwanza ni uwanja wa pili unavyohudumia idadi kubwa ya abiria wa ndani nchini
ujenzi na ukarabati wa Mwanza Airport umefikia wapi?
 
Wasiposhusha nauli za ndege kama Fastjet hizo route ni upuuzi mtupu.

Watanzania tunahitaji SGR kuliko hizo ndege za kutoza nauli zisizoendana na pato la Mtanzania.

Swali la Msingi Fastjet waliwezaje?
 
Back
Top Bottom