Air Tanzania yapata hasara ya TSh. Bilioni 580 katika kipindi cha Miaka 9

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zimeendelea kuonesha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limeendelea kupata hasara tangu Serikali ilipoamua kulifufua kwa kununua ndege mpya kadhaa.

Air Tanzania na hasara zake miaka 9 mfululizo

2014/2015 - Tsh. Bilioni 94.3
2015/2016 - Tsh. Bilioni 109.2
2016/2017 - Tsh. Bilioni 113.8
2017/2018 - Tsh. Bilioni 26.6
2018/2019 - Tsh. Bilioni 48
2019/2020 - Tsh. Bilioni 60.24
2020/2021 - Tsh. Bilioni 36.2
2021/2022 - Tsh. Bilioni 35.2
2022/2023 - Tsh. Bilioni 56.64

Ukijumlisha hasara jumuifu (accumulated losses) ya Air Tanzania Company Limited (ATCL) hadi kufikia mwaka 2022/2023 jumla ni TSh. 580.18 bilioni.

 
Na bado hasara zina endelea mwaka hu, kwanini wasikadhi hilo shirika fastjet wana uwezo waache kushupaza shingo hizo ni pesa za watanzania.
 
Na bado wanaongeza gharama za tiketi kila kukicha
Hawana plan B wanatawaluwa pride badala biashara, kuna nchi nyingi hazina mashirika ya ndege au waingie ubia na private kama fastjet ili waepuke muendelezo wa hasara.
 
Hizo peza ni bajeti ya mwaka zamanisipa za wilaya zaidi ya 20 Imagine, kwanini hilo shirika liendelee?
 
Kila siku shirika linaendeshwa kisiasa kwa matakwa ya mama na safari zake, litaachaje kupata hasara? Ni ujinga kama huu ulisababisha Raisi Zuma wa South Africa kuiua South African Airways
 
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Hasara inajetegemea kila mwaka au inakuwa "carried forward"?
 
Kikubwa tukae Kwa kutulia. Tuendelee kumshangilia kocha huyu wa kike wa Yanga na timu yake
 
Kuna mtu alitarajia faida kutoka ATCL?
Mwendo kasi chali
ATCL chali
TTCL chali
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…