Airtel 5g: Ni kasi ya mtandao au ni kasi ya kuiba pesa za wateja?

Airtel 5g: Ni kasi ya mtandao au ni kasi ya kuiba pesa za wateja?

baharia 1

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
3,016
Reaction score
4,404
Malalamiko kwa Airtel Tanzania: Huduma ya 5G au Tapeli.

KWA WATEJA WA AIRTEL 5G ROUTER – ACHENI KUPOTEZA PESA ZENU!

Nimekuwa nikitumia huduma ya Airtel 5G Router kwa miezi kadhaa sasa, nikilipia Tsh 70,000 kila mwezi. Miezi ya mwanzo huduma ilikuwa inaridhisha, lakini sasa imekuwa ni kero na utapeli uliopitiliza.

Hoja zangu za msingi:

Ninalipia lakini sipati huduma: Kila mwezi ninaweka 70,000, lakini intaneti haifanyi kazi kabisa. Hata kufungua ukurasa wa YouTube ni mtihani. Je, hii ndio 5G mnayoinadi?

Ubaguzi wa Kifaa:

Inakuwaje intaneti kwenye simu inakubali kwa kasi, lakini kwenye Router mliyoniuzia huduma inakuwa mbovu? Huu ni uhuni wa makusudi ili watu waendelee kununua MB za simu wakati tayari wameshalipia Router?

Wizi wa mchana: Kuchukua 70,000 ya mteja bila kumpa huduma inayostahili ni utapeli. Huwezi kuita hii ni "huduma ya jamii" wakati unanyonya wateja wako bila aibu.

Tahadhari kwa Wadau na Wateja Wengine:

Kama unataka kununua router ya Airtel, FIKIRI MARA MBILI. Utapoteza pesa zako na utaishia kupata maumivu ya kichwa. Ni bora kutafuta mbadala kuliko kuendelea kulisha kampuni inayodharau wateja wake kiasi hiki.

Ujumbe kwa Airtel

Msinitumie meseji za Template za kuomba radhi. Ninataka huduma niliyolipia ifanye kazi, au rudisheni pesa yangu. Hamuwezi kuendelea kuchukua hela za watu kwa huduma hewa

#AirtelTanzania #Airtel5G #Utapeli #HudumaMbovu #Tanzania #TCRA

Airtel Tanzania, acheni njaa! Mnachukua 70k ya mteja halafu mnamzimiia intaneti? Hii Router yenu ni takataka, Mtu anajinyima ili apate huduma, nyie mnaichukua hela kama sadaka bila kutoa huduma. Kama hamtaki kufanya kazi, rudisheni hela za watu. Mmetuchosha na utapeli wenu wa 5G ya mchongo

NIMEMALIZA [emoji35][emoji35][emoji35]View attachment 3587217
IMG_20260511_195839_652.jpg
 
Hivi wizi wa aina hiyo hauwezi kuingia kwenye jinai?
Ni kwakuwa TTCL imefubazwa na wapenda rushwa vinginevyo wote tungehamia huko kuepuka uhalifu wa wazi wazi.m kama huo.😳
 
Hivi wizi wa aina hiyo hauwezi kuingia kwenye jinai?
Ni kwakuwa TTCL imefubazwa na wapenda rushwa vinginevyo wote tungehamia huko kuepuka uhalifu wa wazi wazi.m kama huo.[emoji15]
Ni jinai kabisa! Huwezi kuuza bidhaa mbovu kwa bei ya dhahabu na bado ukaendelea kuchukua malipo ya kila mwezi huku ukijua huduma haifanyi kazi. Airtel wanatakiwa kushtakiwa kwa utapeli huu.
 
Me napata average hii
IMG_8565.png

Unatumia ile ya box au ile ya kufunga nje?
 
SIJAWAHI KUONA TOFAUTI YA 3G, 4G,na 5G kwenye internet au mawasiliano ya simu
 
Wabadilishe nn sasa wakati hamna mtandao na linawaka
1. Toa laini kwenye hilo box alafu iweke kwa simu ndogo au simu yako yoyote then piga *106# angalia usajili, ukiona inakwakwambia laini haijakamilisha usajili hilo ndiyo tatizo... (Hata kama ulisajili kwa alama za vidole hizi laini za SMEs za router za Airtel zinapoteza sana usajili baada ya muda ndiyo hupelekea hilo tatizo laini haipandi data na taa ya internet haiwaki)

2. Ikiwa laini haina shida weka laini kwa box alafu set 4G Only au Auto, usiweke 5G Only hii huwa inapotea potea sana ukiwa sehemu yenye mawimbi ya 5G dhaifu, so weka tu 4G inatosha sana kwa matumizi ya kawaida...
 
Naset vp sasa
 
Back
Top Bottom