Airtel, huduma kwa wateja ni mbovu - wanakesi CMA na watoa huduma wao

LUPANGO

New Member
Joined
Feb 20, 2013
Posts
2
Reaction score
0
Habari wanajamvi
Nimekuwa nikipiga simu huduma kwa wateja Airtel mara nyingi na kwa kweli mara zote nakutana na madudu na majibu ya watu ambao nazani hawajui wanachokifanya. Kumbe TCRA wamewa rank wa mwisho kwenye kutoa huduma nzuri za kumtosheleza mteja ( customer satisfaction survey ) uku Voda na Tigo wakiwa ni vinara.

Ila nimejaribu kufuatilia nkagundua tatizo ni hao wafanyakazi ni kama wamechoka na kazi hao maslai yao sio mazuri, nlichoka nliposikia jamaa wanalipwa kiduchu mno kiasi cha kuwafanya wawe na kama na kimgomo baridi hivi. Lililo nichosha zaidi nikusikia eti baadhi ya wafanyakazi wamefungua kesi itakayosikilizwa tarehe 4 mwezi March pale CMA wanadai malipo ya kusitishiwa mkataba na kupelekwa kampuni nyingine inaitwa SPANCO.Naskia hao wakenya wamegoma tena wanadai nyongeza ya mishahara
. Anayebisha kuhusu huduma mbovu apige 100,170 au 500 aone majibu yake kama hajaambiwa azime simu awashe au system yangu iko chini kata piga tena na kero nyingine nyingi.

MY TAKE: Kama kampuni inafikia mahali pa kushtakiwa na wafanyakazi wake wanaohudumia wateja sisi wateja si ndio tutakaokuwa tunaambulia matusi kila kukicha.
 
Hata kamisheni yao kwa tunaotoa huduma ya airtel money ni ndogo sana kiasi kwamba hata mteja akija unamhudumia kwa kuangalia kiasi cha float uliyokuwa nayo kwani usije ukaweka hela nyingi kwenye airtel money ukashindwa kuhudumia wateja wa mitandao mingine ambayo inafaida nzuri. Inawapasa kuangalia vizuri utendaji wao kwani wanapoteza wateja wengi sana kila kukicha sisi tuliokuwa huku sokoni tunaona ila hatuna jinsi kwani na sisi tunaangalia faida so hata treatment ya mteja ambaye anatumia airtel inakuwa hafifu kwani hatupati kinacho stahili na isitoshe wanachelewesha commision na unaweza kukuta umehangaika nao mwezi mzima unapata 15,000 sasa hebu angalia utaweza kulipa japo mfanyakazi kwa faida ndogo kiasi hiki na umewekeza mtaji wa milioni mbili au zaidi. AIRTEL TANZANIA kuweni serious na biashara zenu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hawa wa Arusha kwenye upande wa corporate clients ndio Noma balaa.
Wapo wawili pale gorofani wamefana tabia mwanzo mwisho.
Wana dharau na ubishoo, wavivu kinoma, majibu ya kipuuzi na hawan idea ya ni kitu gani wanafanya.
 
hao wafanyakazi nao hawana akili wamegundua wanalipwa kidogo kabla ya kuomba kazi au baada ya kupata kazi ni kweli airtel huduma zao ni mbovu customer care ni kama hakuna
 
You guys, Airtel wako hapa kuchuma mapesa na kuondoka, hawako hapa kutoa huduma ya maana; airtel ni kampuni ya kutoka India,

Wamefinya bajeti ya matangazo; wanawalipa wafanyakazi kiduchu, activities zao za corporate responsibility ni finyu sana kulinganisha na makampuni mengine katika revenue bracket yao.; rates zao za billing hazitabiliki; nk nk.

Airtel wako hapa kwenye shamba la Bibi to hit and run, expect no more! and sooner rather than later you will here them no more; watauza kampuni na kuyeya kama Celtel na Zain watangulizi wao.
 
mi nlishawahi kupiga na nlishangaa kuskia kelele kwa upande wa nnae ongea nae kunipa huduma,yani kama alikua kwenye watoto wa darasa la kwanza
 
Uozo huu sasa wafanyakazi wanawaburuza mahakamani wanadai chao vikampuni vya kihindi bana vimejaa umaskini na hujuma tu, kwanza nasikia ajira zenyewe huko huduma kwa wateja siku hizi waombaji wananunua unatoa hela ndio upate ajira, yaani upuuzi mtupu sasa mtu aliyenunua kazi atatoa huduma nzuri. Wahindi wamulikwe hawa wezi sana. Airtel wanachefua sana

Sent from Samsung tablet
 
Sijawahi kuona customer care mbovu kama ya hawa airtel,mpaka unajisikia hasira
unaomba msaada kuhusu modem,mtu anakujibu kama darasa la 2
ukimuongelesha kimombo ndo kabisa anatupa mkonga wa simu.
This is TZ
 
Naskia shauri lao ni Jumatatu ya tar 4 saa nne asubuhi pale CMA................
 
Niliwahi kuweka uzi hapa jinsi AIRTEL wafanyakazi wake wanposhiriki kuhamisha salio la mteja.Kampuni hii inaelekea kubaya!!!!!!!!
 
Eti hamia airtel, yani tuamie kwenye upuuzi?
Tangu walipositisha bundle ya internet ya mb 400 kwa 2500 nimeivunja line ya airtel nimetupa mbali kabisa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…