Airtel huduma ya INTERNET imepatwa na nini? Mboni hali hii haikua hivi imekuaje?

Airtel huduma ya INTERNET imepatwa na nini? Mboni hali hii haikua hivi imekuaje?

Ambivert88

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
3,609
Reaction score
6,388
Wakuu.

Nimewaita mara moja, mimi ni mdau mzuri wa mitandao ya Simu hususani mtandao pendwa wa Airtel ila kwa siku za hivi karibu mtandao wa Airtel umekua na sintofahamu hususani kwenye upande wa Internet, nataka kuwauliza wahusika kimetokea nini?

Mtandao wa Airtel umekua mziiiiiiiiiito ninaposema mziiiiiiiito namaanisha mziiiiiiiiiiiiiiiiiito kwenye upande wa Internet yaan ukitaka kufanya shughuli zako za fasta fasta Airtel itakufelisha maana inakutaka usubiri, week hii imenipotezea hela mara nyingi maana wasichoelewa kasi ya mtandao kwa baadhi ya watu ni pesa siku hizi yaan mtandao ukiwa hauna kasi watu wanapoteza pesa ni sawa na kukatika kwa umeme wa TANESCO kuna watu wanapoteza pesa gizani.

Airtel Internet kunani? Nini shida?

Nisingependa kuongelea mitandao mingine maana Halotel nimewaacha kabisa situmii Internet kwenye Halotel waliobakia Vodacom nao ndio km Airtel ila tofauti ya Vodacom ni moja tu pamoja na kukwamakwama kwao mara kadhaa ila mtandao una kasi haugomigomi km Airtel na nikitumia Vodacom napiga hela vizuri tu ila Airtel inanifanya napoteza hela sababu kasi kasi yake ni ndogo pesa zinanipita.

Usiulize napoteza hela kivipi wewe elewa hio bando yako km unaitumia kupost vitu WhatsApp statuses na kutembelea Insta na YouTube kuna watu wanaitumia kuingiza hela 24/7, sasa mtandao unapokua wa manati unagomagoma pesa zinaenda tunapoteza pesa kwa mtandao usio na kasi ya Internet. Tigo Yas ni Mix by Yas at least kidogo ingawa siitumii sana ila haiko vibaya kwa upande wa Internet km Airtel.

Airtel Internet imepatwa na nini? Nini kimetokea?
 
Back
Top Bottom