Nadhani Tanzania kuna shida sana kwenye utoaji wa huduma.
Kidogo Voda wapo vizuri sio mitandao ya simu tu Bali hata kwingineko ni hovyo hivyo tu.
Siyo huko tu hata kwenye hoteli
Na hata unaposafiri utagombaniwa tu pindi hujakata ticket
Ukikata then upate changamoto hawana habar nawewe Tena mara kaa hapo subiria kwanza nk .....
Hii imechangiwa na kupeana kazi Kwa kujuana yaani kuangaliana usoni kuwa huyu wa ba mdogo huyu wa shangazi ama wa dada nk.
Nilkopa mtambo wa Sola wa kuwa nalipia Kila mwezi kiasi fln
Siku Moja nikafanya makosa ikabidi niwapigie. Alipokea mwanaume nikamwelezea shida yangu then akasema subiri tusikate simu niangalie nitakurudia Hivi punde.
Simu ilikaa hewan kama dk20 Hivi sijibiwi kitu ikabidi nikate nipigiee tena
Nilipopiga akapokea mwanamke Bahati nzuri yule jamaa jina nilikuwa nishalijua Tyr nikaomba Moja Kwa Moja niongee na fln yule dada akasema ametoka kidogo kama sitojari hata yeye anaweza nisaidia.
Nikajieleza upya yule dada akaniambia vile vile ka sekunde47 tu akatatua shida yangu.
Akaniuliza una changamoto nyingine nikusiadie nikamwambia nahitaji niongee na fln bila huyu kuongea nae Bado nitarudi kupiga simu Hadi nifanikiwe kumpata hata kama sio Leo.
Yule dada akaomba niseme changamoto Ile nikamwambia Kwa hasira sana nikamwambia kama alijiliwa na shemeji yake hapo mwambie ajitafakari sana.
Hata sisi tunafanya kazi za watu na tuna heshimu sana watu haiwezekan anikalishe halafu aondoke bila kunipa taarifa nikae hewani Kwa dk20
Jamaa huyu mwambie ni MPUMBAVU sana. Hii company sio ya dadake.
Dada akaniomba samahani sana ni kimwambia hakikisha unalifikisha hili sehem husika.