Airtel Kwa hii spidi yenu ya internet HAPANA

Airtel Kwa hii spidi yenu ya internet HAPANA

Nilidhani ni mimi peke yangu naliona hili, kwa kweli aritel kwenye internet wanatia aibu sana nafikiria kung'oa nanga kwa kweli. Usiombe uwe unasafiri upo kwenye basi, hawashiki kabisa sio internent,
voice au sms.
 
Sijui airtel wana shida gani sasa hivi 🤨🤨
20200323_201809.jpg
 
Kwa kweli ninahuzunika sana

Inakuaje mnakuwa na internet slow kiasi hiki? Iwe mjini au pembezoni kote ni Jau kabisa.

Fanyeni kitu bwana nyie ni mtandao wa watu wazima mnatakiwa muwe na mambo mazuri. Mnashindwa nini sasa?

This is too much.

Hii post nimeanza kuandika sijua saa ngapi ila ndo inaenda hewani sa hivi?

Wenye Mawasiliano ya Airtel Waambieni. Kesho nitawapigie huduma kwa wateja niwaeleze dukuduku langu.
Wwako hivyo huwa situmii kabisa
 
Mzee Aitel walianza kwa kasi, nikasajiri line mbili kwa mpigo, nikawa najaza bando za mwezi, ikizima cm moja nachukua nyingine!

Kilicho nipata nakijua mimi! Ilibidi nisajiri laini ya voda G4!

Mzee nakula bata kwa raha zote.
Vodacom kazi nikwako. Na
Yajayo yanafurahisha.
 
Voda wanashida ndogo ndogo ila kwa internet aah wako vzr sana!
Waulize Tigo watu walitekwa sana tigo nikawaambia tigo nawajua sana nawapa miezi mitatu tu.
Kweli waulize watu watigo na vifurushi vyao km vipo.
 
Nilidhani Airtel ni mkombozi baada ya kuhama kutoka Halotel, maana Halotel wamenizingua katika suala la 4G wananiambia line ina 4G wakati sio kweli. Mwanzo nilipo kwenda katika ofisi yao waliboresha line vizuri na ilishika 4G vyema baada ya muda kidogo ikawa haikamati 4G kwenda ofisini wanasema 4G ipo kwenye line! na kuniambia sababu ni maeneo niliyopo likiwemo na la kwao hayana 4G kitu ambacho si kweli maana kuna jamaa anatumia line ya Halotel iliyofanywa maboresho na tupo eneo moja kwake ipo vyema. Nilipoona hali hiyo nikasema ngoja nihamie Airtel labda kuna unafuu, kuja Airtel naona nao mizinguo zaidi ya Halotel maana kama 3G/4G zinashika lakini spidi ndogo!. Vodacom wanagharama lakini huduma zao sio haba hata kama unatoa fedha nyingi kwa ajili ya data lakini unafaidika na spidi nzuri hakika wana 4G yenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom