Watanzania tunapenda sana majibu mepesi,ajabu hata waliopita shule nao wameishia kukimbilia kusema ufisadi huku wengine wakiimba wimbo wa Freemason.
Kenya bei ziko chini na huduma ni nzuri kwa sababu wana-enjoy economies of scale,uchumi wao ni mkubwa kuliko wetu na pato la mwananchi ni kubwa kuliko la kwetu.Hivyo Kenya wana-effective demand kubwa kuliko sisi.Sometimes tusikimbilie kulaumu kampuni zinazofanya biashara Tanzania kwani mazingira ya biashara ni magumu.Bado kuna watu wengi tunapenda na kuendekeza sana vitu vya bure-free riders ni wengi mno,angalia 'Wasomi' wetu wa vyuoni na shuleni walivyojazana mtandao wa Tigo ilhali huduma ni mbovu,Wenzetu Kenya kuna mtandao wa YU ni bure kabisa lakini bado umekosa wateja kabisa kwa sababu watu si tu kwamba wanataka huduma bora bali wako tayari na wana uwezo wa kulipia.Shida ya Tanzania ni volume ya wateja wenye uwezo wa kulipia quality service kuwa ndogo kulinganisha na wenzetu wa Uganda na Kenya.