Airtel kwenye bando ni wezi wasio na aibu. Nnape hawezi kutusaidi, tufanyeje?

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Airtel katika bando la internet si wezi tu ni majambazi yasiyo na haya. Nchi hii wananchi wanaibiwa, wananyanyaswa hakuna mtetezi.

Wakubwa hawafanyiwi hivi hawawezi kustuka. TCRA wako pale, waziri yuko pale hawana msaada kwa wananchi. Unaweka bando hata hujatumia unaanza kupokea msgs kuwa bando lako la internet limeisha, maumbwa utafikiri wanakujali kumbe mashetani yasiyo na haya.

Wameona watu wengi wanatumia internet wakawekeza uwizi wao humo. Kwanza zile messages zao ni kero, kwanini ulazimishwe huduma usiyohitaji? Pili wakimaliza kuiba bando lako wanaenda kutumia salio lako kwa nguvu bila ridhaa yao, huu ni ubakaji wa rasilimali ya mtu.

Nani wa kutusaidia? Sijawahi kuwa na imani na Nnape, labda mh. Waziri mkuu. Mbona nchi za watu upuuzi huu siyo rahisi, kwanini Tanzania?
 
Nape ni fundi wa IT?

Kuna mamlaka zenye wajibu wake wa kusimamia matumizi ya bundle
 
Nape mshitakieni kwa Makonda
 
Labda halotel ndo tujaribu kwa bando
Ukitaka kupumzika kidogo na hiyo kero ya mabando, hamia unakokusema ila nunua line inaitwa ya chuo.

Unainunua 6,000/= lakini kila mwezi watakuingizia bonus ya 1500 kwa muda usiopungua miezi 6.

Tukija kwene bando *150*55# utakutana na vifurushi na zawadi.

Sasa hivyo ukiunga wanakungezea %100 ya furushi ulilonunua.

Mimi kwa sasa ndiyo nimegundua hili chaka nashinda nimejificha humu.
 
Je kwa line ya mwanzo unaweza badilisha ikawa ya chuo, na huduma za mabadiliko unafanyia kwenye maduka yao au hata wakala?

Naomba kujuzwa tafadhari.
 
Uko mkweli kabisaaa @airteltz hawatutendei haki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…