Airtel money cross border money transfer

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,418
Reaction score
9,209
Nov 1 Airtel money imezindua huduma ya kutuma,kupokea na kutoa hela nchi za Tanzania, Kenya,Uganda na Rwanda. Waliotumia huduma hii tunaomba mtujuze faida na hasara ya huduma hii muhimu hasa kwa wafanya biashara wadogo.
 
Huduma hii ina faida nyingi kwa wafanya biashara wadogo na wenyeji wa nchi hizi kwa jumla. Mfano, dereva aendeshaye lori kutoka Dar kwenda Rwanda hatahitaji kubeba TZS nyingi mfukoni tena na kuzibadilisha Rwanda Francs kwenye border. Ataziweka tu kwenye mfuko wake wa airtel money na kuzipokea zikiwa kwa sarafu za nchi hio atakapozihitaji. Mfanyabiashara akisafiri kutoka mombasa kuja kariakoo au wa kariakoo kwenda kuuza Uganda atafanya vile vile.
Njia hii ni ya haraka na tena ni salama kwa wananchi hasa wale wasiokuwa na huduma za benki (ambao ndio asilimia kubwa ya wenyeji wa nchi hizi) Faida zingine unaweza ukasoma zaidi kwenye link hii...

Cross-border mobile financial services in Africa: the next big opportunity for mobile operators - Insight - News | Analysys Mason
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…