Airtel Money vs Mpesa - Airtel Kenya Yaanzisha Vita Vya Bei Kutafuta Sehemu Ya Soko

Airtel Money vs Mpesa - Airtel Kenya Yaanzisha Vita Vya Bei Kutafuta Sehemu Ya Soko

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38
1138.jpg
Airtel Money inaonekana kuandaa vita vya bei dhidi ya M-Pesa huku Kampuni inayoshikilia biashara ya Airtel Money katika masoko ya Afrika Airtel Mobile Commerce N.V ikisema itatumia ada nafuu, motisha kwa wateja, muunganiko mpana wa mitandao na kuongeza mawakala kuvuta Wakenya zaidi.

Kwa sasa, M-Pesa bado inatawala soko kwa mbali. Kufikia Juni 2026, M-Pesa ilikuwa na takribani 88.8% ya usajili wa huduma za mobile money nchini, dhidi ya 11.1% ya Airtel Money. Kwa jumla, kulikuwa na karibu usajili milioni 54 wa mobile money.

Lakini Airtel imekuwa ikipakua sehemu ya soko hilo. Miaka 3 iliyopita, Juni 2023, Airtel Money ilikuwa na karibu 2.8% pekee, wakati Safaricom ilikuwa na takribani 97%. Sasa Airtel iko 11.1% sawa na takriban watumiaji milioni 6, ikilinganishwa na takriban milioni 48 wa M-Pesa.

VITA VYA BEI VIMEANZA?
Airtel tayari imeanza kushusha gharama katika baadhi ya huduma. Mnamo Agosti, ilizindua Bizna Wallet, ikilenga wafanyabiashara wadogo kama mshindani wa Pochi la Biashara ya M-Pesa, huku malipo kupitia huduma hiyo yakitolewa bila ada ili kuvutia wafanyabiashara.

Safaricom nayo haikukaa kimya. Mpesa ilipunguza baadhi ya ada za Pochi la Biashara na Lipa na M-Pesa Buy Goods, huku malipo ya hadi shilingi 200 kupitia Pochi la biashara yakiwa bila gharama kwa mteja chini ya mfumo huo mpya.

Kwa hiyo, kile kinachoonekana sasa si tu Airtel kutafuta wateja bali ni ushindani unaoweza kulazimisha M-Pesa kujibu kwa bei, ofa na huduma.

LAKINI AIRTEL INA CHANGAMOTO MOJA KUBWA.
M-Pesa si huduma tu ya kutuma pesa. Ni mtandao mzima ambao Wakenya wameuzoea: mawakala, wafanyabiashara, PayBill, Till, kutuma pesa kwa familia, kulipa bili na huduma nyingine nyingi. Kwa hiyo Airtel inaweza kusema “tutakuwa cheaper”, lakini swali ni:

Je, bei nafuu pekee inaweza kumfanya Mkenya abadili wallet anayoitumia kila siku?

Na kwa upande mwingine, kama Airtel itaendelea kuongeza watumiaji, mawakala na biashara zinazokubali Airtel Money, M-Pesa italazimika kupigania zaidi uaminifu ambao kwa muda mrefu imekuwa nao karibu bila mpinzani wa kiwango hiki?

Hata upande wa mawakala unaonyesha ushindani unaongezeka. Idadi ya M-Pesa agents ilifikia zaidi ya 333,000 mwaka wa fedha ulioishia Machi 2026, huku baadhi ya mawakala wakianza kutoa huduma za Airtel Money na agency banking ili kuongeza mapato.

MWISHO WA “M-PESA NI DEFAULT?"
Huenda si kesho lakini Airtel sasa haionekani kutafuta tu kuwa namba mbili. Inaonekana inataka sehemu kubwa zaidi ya wallet ya Mkenya. Na kama njia yake ni ada ndogo, cashback, ofa na huduma zaidi, huenda mshindi mkubwa wa vita hii akawa mtumiaji wa mobile money.

Je, ikiwa Airtel Money itakuwa nafuu kuliko M-Pesa, wewe uko tayari kubadilisha au M-Pesa imejikita sana kwenye maisha ya Mkenya kiasi kwamba bei pekee haitoshi kuhama?
 
Back
Top Bottom