Sultani Makenga
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 621
- 1,039
Nimekuwa mteja wa huu mtandao tangu mwaka 2006 ulipokuwa ukijulikana kwa jina la Celtel mpaka leo. Inasikitisha na inaudhi mno kuona kwamba huu mtandao uliotokea kupendwa sana na watu wa vijijini kwa huduma nzuri kipindi cha nyuma ndio mtandao unaoongoza kwa huduma MBOVU KABISA siku hizi.
Ukipiga simu usikivu ni sifuri, customer care hovyo utadhani wako kwenye klabu ya pombe za kienyeji majibu wanayokupa ni ya uongo. Njoo kwenye huduma za kifedha yaani airtelmoney na Timiza ndio ovyo mno. Nilikuwa na utaratibu wa kujiwekea pesa Timiza, juzi nikawa na shida nikaamua nitoe kiasi kidogo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ili kutoa pesa ni lazima uitoe hela kutoka Timiza kwenda airtelmoney.
Nimeprocess kutoka juzi jumatano saa 2 usiku mpaka sasa ninavyoandika ijumaa hela haionekani na kila nikiwapigia Airtel huduma kwa wateja wanasema wanarekebisha, huo ni upuuzi na ujinga wa kiwango cha juu, kama walikuwa wanajua kwamba kuna marekebisho si wangetutaarifu wateja tukajipanga.
Hizo pesa tulizoweka kwenye huo mtandao wao wa kipuuzi ni zetu siyo mali zao. Nitavunja hilo li laini lao pumbavu kabisa.