Airtel, please stop this nonsense...

Airtel, please stop this nonsense...

Planett

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2014
Posts
10,497
Reaction score
16,180
Wakuu nawasalimu kwa jina la JMT,

Imekua kawaida sasa kila nikipiga simu ya kwanza (kuanzia saa sita kamili usiku na kuendelea) napokelewa na ujumbe NDUGU MTEJA LINE YAKO HAIJASAJILIWA KWENYE MFUMO WA SPEED YA 4G HIVYO HUTAWEZA KUITUMIA KWENYE 4G TAFADHARI IBADILI SASA UPATE GB 7 BURE. Huu ujumbe unachukua kama sekunde 6 ndio simu ianze connection na ninaempigia. Maswali kwenu Airtel,

(1) Mnadhani sifahamu kwamba line ninayotumia ni 3G?
(2) Mna uhakika sehemu nilipo kuna 4G coverage?
(4) Mkichungulia kwenye matumizi yangu ya internet mshaona mimi ni mdau wa hii huduma?
(5) Mnanipotezea sekunde zangu 6 kuniambia the same ujumbe kila siku kwamba mshaniona mimi popoma hua nikiambiwa mara moja sielewi?
(6) Kama nimeamua kukomaa na 3G hamuoni kwamba nimeamua kujiridhikia na maisha yangu?

Kama huduma ni bora mtu atabadili mwenyewe bila hata kuambiwa, mjikite kwenye kuboresha viwango vya huduma na sio usumbufu huu mnaosababishia watu bila sababu za msingi. Kesho nikikutana na huu ujumbe tena MTANITAMBUA MIMI NI NANI, mark my words.
 
Why mnahangaika na kulialia binafsi sijawahi kujuta na Vodacom Tanzania kwenye bundles,kupiga na kupokea, msgs ukituma inafika muda huohuo, internet hata ikiwa h+ nateleza.

Vodacom kazi ni kwako tu
 
Ila airtel bhana 😂😂 wana matangazo mazuri sana ila sasa kwenye huduma ndo kilio.
Tanzania nzima, mtandao bora ni Vodacom tuu.
 
Kuna siku kuna mmoja kanikera sana, anajaribu kuniaminisha na hiyo 4G yake ili hali hata 3G tu yenyewe haipatikani. Mimi nilishasahau kutumia bando la airtel japo nalinunua kwa kulazimishwa kwa maana ya kuwa ukinunua dakika unaunganishwa MB ambazo huezi kuzitumia hata chembe. Najaribu kumwelewesha haelewi mwisho nikampa za uso. Sasa imebaki kila siku sms za bando lako internet limeisha. Wapuuzi sana hawa jamaa.
 
Natamani niwaone sura zao hata kwa picha watendaji wa Airtel,,,Niishie hapa!
 
Kwenye line yangu inaonyesha kuna sh.1700 kila nikiangalia salio,ila nikitaka tu kujiunga naambiwa insaficient balance
 
Sasa na nyie mnatumiaje airtel? 😂😂😂
 
Ila na wewe saa sita usiku unapiga Simu za Nini? Airtel hawakuelewi
 
Back
Top Bottom