Habari ya asubuhi wana JF.
Asubuhi ya leo imekuwa ni mbaya sana kwangu, mimi kama walivyo wateja wengine wa airtel, nimekuwa nikitumia huduma ya airtel internet, kwa kutumia kifurushi cha 400MB/2500Tsh tangu mwaka 2010. Leo asubuhi nikagundua kuwa kifurushi changu kimekwisha. Basi kama kawaida, nikanunua tena vocha ya Tsh 2500, nikaingiza, nilipo subscribe ile huduma yetu rafiki kwa kutuma neno internet kwenda 15444, nikapata ujumbe ambao sikutarajia kuupata asubuhi hii, ujumbe ulisomeka hivi
"Name:
Number: 15444
Content:
Neno ulilotuma sio sahihi, Tafadhali chagua kati ya :- 10MB,25MB,50MB,150MB,250MB,500MB,1GB,2GB,5GB,15GB,30GB,SIKU,WIKI,MWEZI ama SALIO kwenda 15444.Asante.
Time: 01/03/2012 08:14:49"
Nikajaribu mara kadhaa nikapata ujumbe huohuo. Ndipo nilipogundua huduma yetu hii kipenzi is no more. Kwa hela hiyo hiyo nikajaribu kutuma mwezi, nikaambiwa hela haitoshi, nikajaribu wiki, nayo nikaambiwa hela haitoshi. Ndipo nikatuma 10MB ambayo naitumia hivi sasa na muda si mrefu itaisha.
Naomba kuchukua wasaa huu kuwaomba ndugu hawa wa Airtel kuirudisha huduma hii, kwani imewakusanyia wateja wengi wa internet ambao wengi watalazimika kuachana na huduma zao kama ile huduma wameiondoa. Mimi binafsi nina modem ya mtandao mwingine wa hapa TZ lakini niliichakachua ili niweze kutumia airtel kitu ambacho ni faida kwa airtel.
PLZ AIRTEL THINK TWICE!!
BAD DAY!!