Airtel Tanzania yapandisha gharama za internet!

Airtel Tanzania yapandisha gharama za internet!

Status
Not open for further replies.
Duh, basi tena. Ngoja nikibanebane kiporo changu cha Mb320, kikiisha natafuta mtandao mwingine au NACHAKACHUA. Si wametaka wenyewe?
 
Duh! Mi natumia airtel kwa ajili ya ucheap ingawa wakati mwingine iko slow! Hapa itabidi nianze kutafuta uelekeo mwingine
 
Nina Blackberry latest vision, nilipokwenda Voda kuwauliza ni kwa nini haiconnect Internet wakanijibu mpaka niwe na BB subscription ambayo gharama yake ni shilling 30,000 kwa mwezi, nikawasihi kwamba hii sio Blackberry yangu ya kwanza kutumia bali ni ya nne nazote hizo nilikuwa nalipia pay as you go, wakaniambia eti sasa hivi mpaka uingizwe kwenye Blackberry server yao na hakuna jinsi ni lazima nilipie 30,000. nimekataa siwezi kujiingiza gharama ambazo ni unneccessary, ni kwa nini laptop yangu nitumie gharama nafuu halafu smartphone ndio inigharimu?

Sasa basi kama hawa Airtel nao watakuwa wameingia kwenye upuuzi wa kusitisha huduma hii rafiki hakuna chaguo lingine zaidi ya ku boycot mtandao wao for good. Watanzania tusikubali kugeuzwa makondoo na mkumbuke zamani tulikuwa tunalipia airtime kwa dolar, ikaja tukawa tunachajiwa kwa dakika na hatimaye sasa tunachajiwa kwa sekunde, pls kama hili swala ni kweli tutaanzisha special thread hapa na kukusanya chip zao tuwarudishie na uzuri media tunazo humuhumu.
 
Duh! Mi natumia airtel kwa ajili ya ucheap ingawa wakati mwingine iko slow! Hapa itabidi nianze kutafuta uelekeo mwingine
Kama naanza kunusa harufu ya ukweli wa habari hii, maana nimeangalia salio langu sasa hivi hata ile style yao ya kuone salio wamebadilisha. ona inavyoandika.
Name:
Number: 15444
Content:
Ndugu Mteja Salio lako ni: 1. BUNDLE : 267MB
Time: 01/03/2012 12:07:12
 
Sasatel nao wamesitisha modem za simu ya mezani na modem zinazotumia line za sim card. Tutaumia wengi!
 
ukitaka kujiunga na kuona salio bonyeza hivi *154*44# halafu unafuatisha kama ilivyo tigopesa au mpesa then you are done!

fanya hivyo iliuzoee..
 
Duh!hv kumbe hizi modem zinachakachulia!!!
Jf ni noma,naaply now now kitendo bila kuchelewa itabaki kubadilisha chip tu basi!!!
 
uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii hii ni bad newz kwangu
 
Sasatel nao wamesitisha modem za simu ya mezani na modem zinazotumia line za sim card. Tutaumia wengi!

Mkuu hebu fafanua, wamesitisha tangu lini? Na nini hatma ya tulionazo?
 
Wakuu jana mida ya saa tatu usiku nilikuwa na salio la mb20 katika bundle yangu ya mb400 nikawa nadowaload kitu cha mb 300 lakini chaajabu nikadownload hadi mwisho, ni nilipo jaribu kuangalia salio nikapata ujembe usemao "Samahani,huduma haipatikani kwa sasa kwa sababu tunaboresha mitambo yetu.Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.Asante".
Nikazima pc na baadae kama saa 7 hivi nikawasha ili nitumie zile mb200 za ofa ya usiku ikakataa kuconnect yaani haina salio
Leo asubuhi najaribu ku activate kifurushi cha mb400 kwa kutuma neno INTERNET kwenda 15444 lakini napokea ujumbe ufuatao " Neno ulilotuma sio sahihi, Tafadhali chagua kati ya :- 10MB,25MB,50MB,150MB,250MB,500MB,1GB,2GB,5GB,15GB,30GB,SIKU,WIKI,MWEZI ama SALIO kwenda 15444.Asante.
Nimechek na website yao bado wanamaelezo ya bundle za zamani
Inakuwaje hapa wadau
 
Sijui kama ni kweli, mimi nimerecharge jana usiku na ikakubali na ndo natumia hadi sasa, wakiitoa hiyo huduma mpango mzima utahamia Zantel, voda na tigo wezi siwataki
 
Labda wameona wanakula hasara bundle ya 400MB ndiyo maana wamebadili.
 
Yawezekana ni kweli, nimeuliza salio wamajibu hivi ambavyo si kawaida
Name:
Number: 15444
Content:
Ndugu Mteja Salio lako ni: 1. BUNDLE : 382MB
Time: 3/1/2012 12:41:54 PM
 
Wakuu jana mida ya saa tatu usiku nilikuwa na salio la mb20 katika bundle yangu ya mb400 nikawa nadowaload kitu cha mb 300 lakini chaajabu nikadownload hadi mwisho, ni nilipo jaribu kuangalia salio nikapata ujembe usemao "Samahani,huduma haipatikani kwa sasa kwa sababu tunaboresha mitambo yetu.Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.Asante".
Nikazima pc na baadae kama saa 7 hivi nikawasha ili nitumie zile mb200 za ofa ya usiku ikakataa kuconnect yaani haina salio
Leo asubuhi najaribu ku activate kifurushi cha mb400 kwa kutuma neno INTERNET kwenda 15444 lakini napokea ujumbe ufuatao " Neno ulilotuma sio sahihi, Tafadhali chagua kati ya :- 10MB,25MB,50MB,150MB,250MB,500MB,1GB,2GB,5GB,15GB,30GB,SIKU,WIKI,MWEZI ama SALIO kwenda 15444.Asante.
Nimechek na website yao bado wanamaelezo ya bundle za zamani
Inakuwaje hapa wadau

Mkuu hawa wehu tu. Naona wamefanya kimya kimya.
Ngoja tusubiri na usiku tuone kama nako wamebana.
 
wamebadili jinsi ya kuangalia salio au kununua kwa kutumia hii njia *154*44# ndio utafanikiwa mi mwenye leo imenisumbua mpaka ikakubali kwenye saa 2 asubuhi..
 
nimepiga simu katika namba 100 wamenitumia ujumbe huu:

"Mpendwa mteja! Kifurushi hiki kinagarimu shilingi 2,500/= tu kwa mwezi. Kujiunga SMS INTERNET kwenda 15444. Utaweza jiunga tena mara umalizapo kifurushi chako"
 
Poleni wapendwa...huduma iyo haijasitishwa bado ipo na itazid kuwepo...leo asubuh kumekuwa na tatizo la netwk kwa baadhi ya mikoa apa nchini poleni sana kwa usumbufu uliojitokeza!

Kwa hiyo wewe ndio msemaji wa kampuni,sio?
Sasa mbona tusipewe taarifa mapema?
 
to Buy new bundles dial *154*44# hayo ndiyo maneno yao..
 
wamebadili jinsi ya kuangalia salio au kununua kwa kutumia hii njia *154*44# ndio utafanikiwa mi mwenye leo imenisumbua mpaka ikakubali kwenye saa 2 asubuhi..

bei ni ile ile...??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom