Airtel yatoa bilioni 32.9 kama gawio na mchango maalum wa maendeleo

Airtel yatoa bilioni 32.9 kama gawio na mchango maalum wa maendeleo

yuda75

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
520
Reaction score
1,412
jamani nikisema pesa ya kampeni hakuna hali mbaya tunabisha aya sasa
magawio yameanza na mtasikia makampuni mengi yakitoa magawio kipindi ichii
sasa sijui hali itakuwaje after election

tuchague sera bora na zinazo tekelezeka na sion vinginevyo

AMKA KITAA BADOO KUNA UTAWALA WA NJAA

=====


====

SERIKALI imepokea hundi ya gawio kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel la Sh Bilioni 32.9 ambapo Bilioni 18.9 ni gawio kwa serikali kwa mwaka huu na Bilioni 14 ikiwa ni mchango kwa serikali kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Gawio hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel, Gabriel Malata na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James leo jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi hiyo, Katibu Mkuu Dotto James amewashukuru na kuwapongeza Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Airtel kwa kuhakikisha gawio linalipwa serikalini na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuwetea watanzania maendeleo.

Dotto amezihimiza kampuni zingine ambazo serikali ina hisa hata kama ni asilimia moja kuhakikisha zinajiendesha kwa ufanisi na kulipa gawio stahiki serikalini.

" Nawapongeza sana Airtel kwa namna ambavyo mmejitoa katika kuiunga mkono serikali yetu na kuenda sawasawa na makubaliano yetu, gawio la Bilioni 32 limewafanya kuwa kampuni ya kwanza ambayo serikali ina hisa nayo kutoa gawio kubwa la namna hii.

Nitoe wito kwa mashirika ya umma na kampuni ambazo bado hazijatoa au zile zinazotoa gawio dogo zijitathimini na kuhakikisha zinafanya vizuri na kulipa gawio serikalini ili kuiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake ipasavyo," Amesema Dotto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel, Gabriel Malata amesema wao kama wabia wa serikali wataendelea kushirikiana katika kuwaletea maendeleo watanzania.

Amesema Airtel imeendelea kuchangia shughuli za maendeleo kwa kutoa kiasi cha Sh Bilioni 2.3 kusaidia ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma ambayo itaenda kuwa msaada mkubwa kwa watanzania.

" Tunajitahidi kuendelea kuwa mojawapo ya Kampuni zinazogusa maisha ya watanzania wenzetu, ndio maana tumetoa ajira rasmi 500, ajira mwambata 350,000 kupitia uuzaji wa vocha na huduma za kifedh.

Pia tumeingia makubaliano na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ambapo tumeanzisha programu inayoitwa V Somo inayowezesha wanafunzi kusoma bila kwenda darasani na mpaka sasa wanafunzi 17493 wameshajisajili," Amesema Malata.


Nae Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Zainab Chaula amempongeza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha kwa ufanisi wake katika kusimamia urejeshaji wa gawio hizo huku akizitaka taasisi zingine kuiga mfano wa Airtel.


 
Kutokana makubaliano yaliyozaa mgawanyo wa hisa asilimia 51 kwa Airtel na 49 kwa Serikali kupitia msajili wa hazina, atakuwa anapata gawio la bilioni 18.99 kwa mwaka pia Airtel Tanzania PLC itaendelea kuchagia michango na mpaka leo imechangia bilioni 14 ambapo itakuwa ikichangia bilioni 1 kila moja.

Airtel imeweza kuchangia kodi mbalimbali bilioni 237. Airtel imelipa gawio kubwa zaidi kuliko kampuni yoyote inayosimamiwa na msajili wa hazina.
 
Viva magufuli, another ten years.q[emoji1360][emoji1360][emoji1241]
 
Haya ngoja tusikilize wanainzengo wanasemaje
 
Back
Top Bottom