Aise wakuu UKIMWI ni noma

Imekuchukuwa miaka mingapi kugundua hili jambo ambalo liko dhahiri na limekuwa likisemwa kwa miaka zaidi ya 30? Wewe ni aina ya wale watu ambao ni lazima waone madhara ndiyo wanakubali?
 
Wanasema sikuhizi ukimwi ni kama mafua,
Usiamini, wanaosema ni wale wasio ugua..

Wewe ukihisi unataka kuwamaliza mabinti wazuri wote, tambua Mungu hajachoka kuwaumba..

Ukitaka kila anayekuchekea upite nae, utakosa wa kulia nae wakati ambao hakuna utani wa kukuchekesha, umekonda unagofya

Kama wewe fahari yako ni kuwasimulia wana jinsi unavyo waumiza..

Kesho itakosekana leso kwaajili ya machozi ya dada yako, kwa kuumizwa vilevile..

Leo wanakusifia kwa kupiga kila mitandaoni huko

Siku nyingine watakusifia kwa kumaliza uji bila kutapika, stuka...

Sikia mwanangu, Zipu mbovu..

Watu wanaumwa na wana hasira kwa kuambukizwa.

Na furaha yao iliyobaki ni kuusambaza ugonjwa katika namna ileile waliyoipata wao.

Wewe jifanye kanyaga twende, tutakuzika na kilo 13, kama kiroba cha sukari..

Chagua manzi moja isiyokupa miwasho na fangasi, ishi nayo afu fanya maisha..

Nawahusia na kuihusia nafsi yangu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…