Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Nilipita njia hiyo kwa dharura kwa sababu daladala niliyopanda ikitokea Mwenge kuja Tabata Segerea ilikwepa foleni, tulipofika Barakuda, tukaingia boda la Chang'ombe.
Huku mwanzomwanzo tumeteleza vizuri, ila kufika mbele, tukakutana na mashimo barabarani, barabara haijakamalika kujengwa hadi mwisho.
Sikuwa nimeenda Tabata Chang'ombe kwa muda mrefu, nilidhani barabara itakuwa imejengwa freshi hadi mwisho kwa sababu nikipita Barakuda naona lami. Kumbe sio.
Bado barabara imekuwa kero sana, mashimo yanaharibu vyombo vya moto.
Kibaya zaidi ni kwamba, hadi leo hakuna stendi ya daladala, magari yanapaki pembezoni mwa barabara kusubiri abiria. Hii ni aibu.
Ukiangalia Tabata Segerea na Tabata Kimanga, kwao safi tu, lakini Tabata Chang'ombe, wapo nyuma sana kimaendeleo unapozungumzia miundombinu ya barabara.
Wahusika oneni aibu, haiwezekani miaka nenda rudi hali ni ileile.