nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 12,106
- 12,916
Kwa kifupi... niliingia humo muda si mrefu...
Lakini ni wazi, pasi na shaka ya aina yoyote kuna faida nyingi mno.
Mimi si mwanachama wa makanisa ya miujiza na mboga mboga.
Nimeokoka kibinafsi chumbani kwangu na Mungu wangu.
Mafundisho nafuata kutoka kwa wachungaji mchanganyiko mitandaoni wanaohubiri kweli na sadaka ninatuma humo humo.
Lakini ni wazi, pasi na shaka ya aina yoyote kuna faida nyingi mno.
- Kiuchumi: Baada ya kutenga sadaka, pesa inayobaki inaniwezesha kukidhi mahitaji. Yaani, inakutana na hesabu ya mwezi unaofuata.
- Kijamii: Heshima inakuja hata kutoka kwa wale ambao hapo awali walinidharau.
- Miradi: Miradi mbalimbali ambayo ilionekana kama imeshindikana au kufa kabisa sasa imefufuka na inafanya vyema, mfano ujenzi.
- Afya: Mwili unakuwa na nguvu ya kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchoka wala kupata kiu ya pombe.
- Mengineyo: Hata mwanamke akiwa amevaa nusu uchi au nguo za kubana, sijielekezi kuangalia makalio yake na michirizi ya chupi kama ilivyokuwa awali.
- Muonekano: Sura (uso) umebadilika, nimekuwa na nuru na uangavu wa kipekee. Nikilinganisha na enzi za 'weka mchupa toa mchupa' a.k.a 'leta kama tulivyo, zungusha round'.
- Amani: Nimekuwa na utulivu wa ajabu ndani ya nafsi yangu kiasi kwamba nina uwezo wa kushughulikia mambo magumu na mazito bila kutoa matusi kama hapo awali.