TANZIA Aisha Madinda afariki dunia

TANZIA Aisha Madinda afariki dunia

Imeandikwa kila nafsi itaonja mauti. na kwa hakika umauti ni mawaidha tosha kwa wenye kuamini.maisha ya duniani ni mafupi sana ila wanadamu tunajisahau sana na maisha haya ya mpito. anza leo kumuabudu Muumba wako usisubiri kesho huenda sasa hivi ndio ikawa pumzi yako ya mwisho.

Jazaka llah khaira kwa ukumbusho
 
‪#‎TANZIA‬ AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA!
Aliyekuwa mnenguaji wa bendi tofauti hapa nchini Tanzania Aisha Madinda afariki dunia na mwili wake wakutwa umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.
Akiongea na EATV Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.
" Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea". Amesema Asha Baraka
Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina source eatv
 
Bado alikuwa ananengua?au unga ulishamchosha kabisa? Rip Aisha.
 
nakumbuka enzi hizo,kila wimbo wa twanga,lazima usikie jina la Fikiri Madinda likitajwa.sijui alikuwa nani huyu mtu.anyway, RIP mnenguaji A.Madinda.
 
Back
Top Bottom