Aisha Madinda tena...

ZionTZ

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2009
Posts
1,283
Reaction score
541
Nimesoma thread ya huyu mnamwita "celebrity" aunt ezekiel...

watu wengi walionyesha kutowakubali "macelebrity" wa kibongo

mi nawaunga mkono sana, em angalieni haya madudu mengine

ya huyu mnamwita "celebrity"....mungu atusamehe...!



Gazeti ‘5 Star’ katika kuhabarisha kwa wakati muafaka, Ijumaa Wikienda, lina maelezo ‘full story’ kuhusu maisha ya Aisha nchini Afrika Kusini na jinsi alivyojikuta akiingia kwenye masahibu hayo.

Gazeti ndugu na hili, Ijumaa, lilikuwa la kwanza kuandika habari ya Aisha kukumbwa na balaa la kufungulia mwaka wa 2010 akiwa Sauzi, katika toleo lake la Ijumaa iliyopita, namba 651, Januari 1-7, 2010.

Ijumaa liliandika kuwa Aisha, akiwa Sauz, amekuwa muumini mzuri wa vitendo vya starehe, ikiwemo kutumia dawa za kulevya, hivyo kujikuta ‘akibebwa’ na wanaume na matokeo yake kushindwa ‘kuukontroo’ mwili wake.

Ijumaa Wikienda linakwenda mbele zaidi kwa kuweka kila kitu kweupe kwamba, wakati Aisha anasafiri kwenda Sauz, alifikia kwa mwenyeji wake wa kike ambaye ni rafiki yake.

Akiwa huko, mbali na mwenyeji wake, pia alikutana na baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini humo ambao walikuwa kampani moja, hivyo kulizoea Jiji la Pretoria ndani ya kipindi kifupi.

Chanzo chetu kinatupasha kuwa, hatari iliyokuwa kwa Aisha ni kwamba miongoni mwa marafiki aliokutana nao, wengine ni walevi wa kutupwa na watumiaji wa mihadarati, kitu ambacho kilizidi kumuweka mnenguaji huyo matatizoni.

“Mimi nilipata bahati ya kuwa naye karibu, kwahiyo niliweza kumshuhudia akitumia kiasi kikubwa cha pombe na kuna shaka kwamba huwa anatumia dawa za kulevya kwa sababu niliambiwa kuwa akiwa Bongo huwa anatumia,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Kingine ni kuwa wakati Aisha ‘anazibuka’ Sauz, kuna Wabongo waliweza kumuona na wakawa wanammezea mate, si unajua akiwa Bongo ni staa? Kwahiyo wao walitaka kuwa naye kwa lengo tu la kuweka ‘chata’, kwenye kumbukumbu zao, ionekane wamewahi kutoka na staa.”

Habari zaidi zinasema kuwa, kutokana na kampani yake mbovu na tabia ya ulevi, Aisha alionekana ni mwanamke ‘luzi’, hivyo wadau wakaanza kuweka mitego kumnasa.

“Hiyo ndiyo sababu ya kumrekodi na kuna video ambazo amerekodiwa akiwa hajijui, lakini nyingine anajua kabisa,” alisema mtoa habari wetu.

Katika ushuhuda wa Ijumaa Wikienda, uchukuaji wa video na picha hizo, umetekelezwa na watu si chini ya wawili, mmoja ni Mtanzania (haina shaka), mwingine raia wa Afrika Kusini, mkazi wa Jiji la Pretoria.

Kutokana na ushuhuda huo, ipo shaka kuwa Aisha alifanya mapenzi na wanaume wawili, Mtanzania huyo na mwenzake Msauz ambao walishirikiana kumpiga picha za video na mnato.

Kwa upande wa Msauz huyo, anaonekana vizuri kwenye video hiyo, lakini Mtanzania yeye anasikika sauti, akimhoji Aisha kuhusu safari yake ya Afrika Kusini na maisha yake kwa jumla.

Wakati sauti ya Mtanzania huyo ikisikika ikimhoji Aisha, mnenguaji huyo anaonekana ‘kideoni’ akijibu maswali yote ya Mtizedi mwenzake kwa hasira.

Aidha, video hiyo inaonesha kwamba wakati Aisha anajibu maswali, ni wakati huo huo anavaa nguo, kitu ambacho kinatoa walakini kuwa na Mtizedi huyo alihusika kitandani na mnenguaji huyo ndiyo maana aliweza kujiamini na kujiachia mbele yake.

Habari nyingine zinadai kuwa Mtizedi huyo na mwenzake wa Sauz, waliamua kumfotoa Aisha, baada ya kumuona ‘amezibuka’, hivyo wakataka kuwapasha habari Watanzania kuhusu staa wao na madudu anayoyafanya nchini humo.

Hata hivyo, chanzo chetu kilisema kuwa kuna uwezekano Mtanzania aliyehusika na mchezo huo, anajulikana nchini ndiyo maana hakutaka sura yake ionekane, wakati mwenzake wa Sauz, yeye aliweza ‘kuuza nyago’.

Mbali na hizo, pia zipo habari zinazodai kuwa, kuna mtu ambaye alipanga kufunga ndoa na Aisha, huyo ndiye aliyegharamia safari ya mnenguaji huyo Sauz na kukumbwa na maswahibu hayo.

Ijumaa Wikienda lilitonywa kuwa, baada ya ‘mchumba’ huyo kuambiwa ameingia ‘choo cha kike’ kwamba Aisha si mwanamke sahihi wa kuoa, aliamua kumpeleka Afrika Kusini ambako alikodi watu, waliompa pombe na ‘unga’ kisha kumrekodi.

“Lengo lake lilikuwa ni kumkomoa kwa sababu ametumia pesa nyingi kumhudumia lakini alichokiambulia ni mateso ya moyo, leo yupo na huyu kesho yule, kwahiyo akamchezea sinema hiyo kisha wakaachana huko huko Afrika Kusini,” alisema mtoa habari wetu mwingine na kuongeza:

“Baada ya kuachana, jamaa akamtimua, kwahiyo Aisha akaamua kuangalia ustaarabu mwingine kwa Wabongo wengine wanaoishi Pretoria, pia yeye mwenyewe alikuwa na akiba ya fedha ndiyo maana hakuadhirika.”

Akizungumza ndani ya video hiyo, Aisha anasema huku akisikitika kuwa watu wanampakazia kwamba alichukuliwa na mwanaume kwenda Afrika Kusini na baadaye akamtelekeza, hivyo hana mbele wala nyuma.

“Najua hayo ni maneno ya magazeti tu, hata Asha Baraka alinipigia simu, akaniambia anitumie nauli ya kurudi nyumbani, mimi nikamjibu kama nimepata nauli ya kuja, nitashindwa nauli ya kurudi?” Anahoji Aisha katika video hiyo.


Chanzo: Ijumaa Wikienda
 
Lazima huyo mdada atakuwa mtamu na hasa kama akipractise yale mauno yake ya jukwaani. Sijui kama huu ukimwi utatuponya
 
haya mapicha sina uhakika kama yana ukweli
Hivi ni lini tutakubali kwamba na wabongo wanafanya mambo kama hayo? Wakifanya wamarekani aaah swafiii...kazi kweli kweli...
 
Kama ni kweli, basi nampa sana pole Aisha. Jamani maisha hayana mteremko. Tusipojifunza kufanya kazi kwa bidii, hii dunia ina watu wanaweza kuwatumia watu wengine pasipo heshima na kuwaacha kwenye wakati mgumu sana.Lakini yote inategemea nini mtu anataka ndani ya moyo wake.
 
Halafu ZEUTAMU ilipokuwa inawamulika mapepe kama hawa bado kuna watu walilalamika.Ule mtambo wa kurekebisha sheria uliwafanya mapepe wajiangalie mara mbili mbili kabla ya kufanya upuuzi wao.
 
Mi nina mtazamo tofauti sana, yawezekana hayo ayafanyayo mwenyewe anayependelea lakini kutokana na kwamba Bongo hatuna utamaduni huo ndo maana akashindwa kuyafanyia hapa nyumbani na kuamua kujisogeza kule ambako anajua hayo akiyatenda hayatakuwa na neno.
 
Na bado naona anakoelekea atatoa cinema ya mavituz ya kikubwa kabisaa
 
Hii ni mara ya pili, mara ya kwanza alitolewa kwenye mtandao akiwa naked, sasa hivi gazeti limesema tena. Sijui kama anaonewa au kuna chembe ya ukweli, taratibu tutajua
 
ni kweli FL , unajua ktk ulimwengu waTechnologia picha sio kitu cha kutilia maanani saana, mtu anaweza kukuchafua muda wowote akitaka.

Kwanini yeye tu kila mara?Tulishaona picha zek za utupu huko siku za nyuma.Hizi za kwenye gazeti la udaku hazihitaji hata ubishi.Okay,watu wanaweza ku-photoshop sura,lakini vipi sura na sauti vifanane?By the way,tunaambiwa mkanda wa video unamwonyesha Aisha Madinda.Badala ya kumtetea ni vema "mnaompenda" mkampa somo la kuuheshimu mwili wake....na ikiwezekana aachwe kubwia unga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…