Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
"Kurugenzi ya Viongozi wawakilishi kwa maana ya Wabunge, wajumbe wa Baraza la Uwakilishi na madiwani na Kamati kuu imemteua Bwana Kayumbo Kabutali ambaye yeye ni Msomi wa Chuo Kikuu na ni Daktari wa mifugo Mbobevu, mwanasiasa wa muda mrefu, amefanya siasa kwenye kabla ya Chaumma akiwa kwenye Vyama kadhaa vya upinzani, amefanya kazi Taasisi mbalimbali kama Mtumishi lakini pia amehudumu CHAUMMA kama Makamu Mwenyekiti Upande wa Tanzania bara mpaka Mei 19, 2025.
Alipoamua kujiuzulu kwa hiari yake ili kutoa nafasi ya kuunganisha na kuborwsha nguvu ya kiungozi na kiutendaji ndani ya Chama chetu. Hatuna shaka yeyote na CV yake kwenye kutekeleza majukumu yake kwenye eneo hilo.
Idara ya mahusiano ya Kimataifa na mambo ya nje, Kurugenzi hii itaongozwa na Rahman Rungwe ambaye ana shahada ya udhamili, kwa maana ya degree mbili, akibobea kwenye masuala ya uchumi na anaongea lugha tatu kwa ufasaha. Anaongea Kiswahili, Kiingereza na anaongea Kirusi kwahiyo ni mtu ambaye tumeamini kabisa atatosha kwa taaluma yake, uwezo wake na ubobevu wake katika masuala ya Kimataifa kuweza kutusaidia Chama chetu kwenye idara hiyo.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mkurugenzi msaidizi kwenye Kurugenzi hiyo ni Aisha Madoga. Huyu anafahamika ni mhitimu wa Sayansi ya Kompyuta, ni mtu ambaye ana uzoefu wa kutosha kwenye masuala ya Kimataifa hasa kwenye ngazi ya mahusiano ya Vyama vya siasa kwenye ngazi ya Kimataifa, ana exposure ya kutosha Kimataifa, ana mafunzo mbalimbali nje ya nchi, amekuwa mkufunzi kwa muda mrefu na ameshika nafasi za kisiasa kwenye ngazi mbalimbali.
Tumeona kabisa Aisha Madoga anaweza kuwa Mkurugenzi msaidizi kwenye Kurugenzi hii."- Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa CHAUMMA akizungumza na wanahabari Mei 24, 2025.