Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Aisha Madoga, amepokea fomu ya kutia nia ya kuwania ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kwa tiketi ya chama hicho.
Madoga amekabidhiwa fomu hiyo na wanachama wa CHAUMMA nyumbani kwake jijini Dodoma Agosti 04, 2025
Akizungumza mara baada ya kupokea fomu hiyo, Madoga amesema ana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Dodoma Mjini kwa uwazi, uadilifu na kwa maslahi ya umma bila ubaguzi.
Aidha, amesisitiza kuwa anaamini kupitia jukwaa la CHAUMMA itamwezesha kufanya kampeni na siasa zake kwa uhuru na amani.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Ikumbukwe kuwa, katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2020 Madoga aliwania Ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akichuana kwa karibu na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Anthony Mavunde (CCM) huku akitajwa kuwa ni miongoni mwa wagombea waliokuwa na umri mdogo