Aishi Manula na makosa yanayojirudia!

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za weekend wakuu,

Ni siku nyingine tena natumai ni wazima wa afya na mnaendelea na majukumu ya kila siku vizuri pamoja na walio mapumnziko.

Wakuu Kuna hili tatizo linalojirudia la huyo kipa anayeitwa (Tanzania one) na hakuna matumaini ya kuisha au kupungua kwani tatizo hili ni la mda mrefu Sana kwa kipa huyu wa club ya SIMBA.

MANULA ni dhaifu sana kwenye mipira iliyokufa (set pieces) na mipira ya mbali ambayo inaonekana Ina mpa shida kwa mda mrefu Sana, udhaifu huo ndio chanzo Cha SIMBA kupoteza michezo ya kimataifa kwa idadi kubwa ya magoli kutokana na tatizo Hilo la mda mrefu linalomtesa kipa huyo.

Jana SIMBA walikuwa na michezo wa ligi kuu dhidi ya MTIMBWA SUGER na kutoka sare ya bao moja kwa moja Ila mazingira ya goli alilofungwa MANULA ni aina ile ile ya magoli anayofungwa kila siku kwa makosa yale ya kutoka golini bila kuangalia movement za mabeki wake.

Hili tatizo ni la defense nzima ya simba kwa ujumla japo MANULA ndo muhanga wa mipira hiyo kwani anakosa, mawasiliano na mabeki Wake, tatizo Kama Hilo lilikuwa lina wasumbua Sana LIVER POOL msimu wa 2017/2018 - japo kuwa wenzetu huwa wana fanya match assessment, na seoson assessment ambapo ni tofauti na kwetu Ila walipunguza tatizo Hilo baada ya kumsajili VIRGIL VAN DIJK msimu ulio fuata na kufanikiwa kupunguza tatizo hilo.

Mlio karibu na kocha wa SIMBA wa makipa mumpe taarifa kwamba CCL zile tano kuna uwezo mkubwa wa kujirudia na zaidi Kama tahadhari zisipo chukuliwa mapema.

By- shabiki wa damu
 
Siku na Ihefu aliokoa magoli mengi ya wazi hakuna aliyehoji ni vema tukaangalia performance ya timu nzima badala ya kushusha lawama kwa mchezaji mmoja
 
Siku na Ihefu aliokoa magoli mengi ya wazi hakuna aliyehoji ni vema tukaangalia performance ya timu nzima badala ya kushusha lawama kwa mchezaji mmoja
Mkuu mbona hapo hamna lawama naongelea tu jinsi anayofungwa kizembe na wakati yule ni goli keeper mkubwa anachezea team kubwa na Tanzania one
Anahitaji kuwa makini zaidi
 
Mkuu mbona hapo hamna lawama naongelea tu jinsi anayofungwa kizembe na wakati yule ni goli keeper mkubwa anachezea team kubwa na Tanzania one
Anahitaji kuwa makini zaidi
Yule jamaa karuka free header na hata kama angebaki golini asingeweza kudaka ila lawama zote kwa Manula.
Hivi uwekezaji uliowekwa pale ndio wa kupata goli moja tuanzie hapo kwanza.
 
Yule jamaa karuka free header na hata kama angebaki golini asingeweza kudaka ila lawama zote kwa Manula.
Hivi uwekezaji uliowekwa pale ndio wa kupata goli moja tuanzie hapo kwanza.
WATANZANIA kwenye suala la mpira tupo nyuma sana kuna team gani ambayo haifungwi au haitoi sare
 
kwamba ile mechi na Ahly angekaa Manuel Neure msingpigwa 5? Kwa beki gani?
Mkuu mbona nime zungumzia mpaka beki hapo juu kwamba hawana mawasiliano mazuri na kipa wao
 
Hivi unafahamu kuwa football ni mchezo wa makosa? Goalkeeper gan duniani hajawahi kufungwa?. Dawa ya kutofungwa kwa kipa ni kuacha kucheza tuuu. MAKOSA YAPO KTK SOKA NA NDIO MAANA MAGOLI YANAPATIKANA

Sent from my SM-N910F using JamiiForums mobile app
 
Lile goli walilofungwa yanga na prison kama angefungwa Manula ungesikia makelele mengi toka kwa washabiki hadi magazetini hata Manula angebaki golini lile lingekuwa goli
 
Manula kichwa kibovu, nahisi hata darasani alikuwa Zerro brain, maelekezo kuhusu hayo mapungufu anaambiwa sana lkn Ovyo kabisa.
 
Ni golikipa bora wa Ligi Kuu ya Bara kwa misimu mitatu mfululizo. Kwa mtu mwenye akili angekuwa ameliona hilo hata kabla hajaanzisha uzi. Tafsiri yake ni kwamba ubora wake (ambao hauanzishiwi uzi hata mmoja) unazidi kwa kiwango kikubwa udhaifu wake (ambao unaanzishiwa nyuzi)
 
Si mzuri kwenye mipira ya juu. Magoli mengi hufungwa lwa mipira ya juu. Labda kikwazo ni height ukilinganisha na ma- goal keeper wengi wa kusasa.
 
Siku na Ihefu aliokoa magoli mengi ya wazi hakuna aliyehoji ni vema tukaangalia performance ya timu nzima badala ya kushusha lawama kwa mchezaji mmoja
Siku Ihefu Manula alikuwa ndio nyota wa mchezo angepangwa Kakonya huyo Barbra wenu angechapwa bakora. Kimsingi Manula anabebeshwa lawama za bure. Timu nzima ni zero. Hata Konde Boy ameshuka kiwango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…