Aishi Manula na makosa yanayojirudia!

Aishi Manula na makosa yanayojirudia!

Siku Ihefu Manula alikuwa ndio nyota wa mchezo angepangwa Kakonya huyo Barbra wenu angechapwa bakora. Kimsingi Manula anabebeshwa lawama za bure. Timu nzima ni zero. Hata Konde Boy ameshuka kiwango.
Hahahaha keyboard warrior sasa konde boy ameshuka kiwango kiaje
 
Mleta uzi nimukuelewa sana japo watu wengi hawakuelewi au hawataki kukuelewa kwa sababu wanazozijuwa wao. Suala hapa ni Manula kufungwa magoli ya aina ile ile kila wakati inapopigwa krosi au kona. Yaani linapokuja suala la krosi na kona Manula hana ujanja kabisa. Pamoja na Manula kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia mashuti ya uso kwa uso anapokutana na washambuliaji lakini isiwe sababu ya kuzuia watu wasizungumzie udhaifu wake mkubwa kwenye mipira ya kona na krosi. Udhaifu huo usipozungumziwa na kufanyiwa kazi na Simba ipo siku watakutana na timu inayopigwa krosi na kona mwanzo mwisho ndio hapa dhahama itakapoanzia hata zile tano tano zinaweza kuwa cha mtoto. Nafikiri kuna vitu viwili hapa aidha kocha wa makipa pale Simba ni bomu au Manula mwenyewe ni mzembe kufanyia kazi yale anayofundishwa na walimu wake kuhusiana na krosi na kona.

Sasa hivi hatuzungumzii tena udhaifu wake wa kufungwa magoli ya mbali kwa sababu amejirekebisha sana kwa kiwango kikubwa.
 
....Nafikiri kuna vitu viwili hapa aidha kocha wa makipa pale Simba ni bomu au Manula mwenyewe ni mzembe kufanyia kazi yale anayofundishwa na walimu wake kuhusiana na krosi na kona.
Kama Manula ni mzembe, unadhani Simba wasajili kipa gani bora anayesubiri krosi hapa nchini?
 
Tatizo sio kufungwa tatizo ni aina ya magoli anayofungwa ni ya aina moja ndo nilichokizungumzia mimi
Ulitaka awe anafungwa magoli ya aina ngapi? Taja:
i).................................
ii)................................
iii)...............................
 
Kama Manula ni mzembe, unadhani Simba wasajili kipa gani bora anayesubiri krosi hapa nchini?
Wakatafute pale Mtibwa walipompata kipa wao labda kabaki mwingine kama yeye. Au wasubiri Yanga wawafanyie "scouting" kama kawaida yao.
 
Wakatafute pale Mtibwa walipompata kipa wao labda kabaki mwingine kama yeye. Au wasubiri Yanga wawafanyie "scouting" kama kawaida yao.
Scouting ya Mtacha na Shikalo hao wa 4G? 🤣🤣🤣
 
Mi nahisi haya makampuni ya sportpesa yanahonga ili watu waliwe,kitu alichofanya Manula ni kama amepanga
 
Kama walishawafanyia "scouting" ya hao waombeni safari hii mna shaida ya kipa watawafanyia tu "scouting" kama walivtyowafanyia ya Beno.
Hakuna kombe wala bingwa anayetangazwa kwa kufanya scouting. Utaishia kujivunia kuwa mimi nipo bora katika scouting, wenzako wananyanyua vikombe kila mwisho wa msimu. Tena hao unaofanyia scouting wanaenda kujiunga bure kabisa, sasa sijui faida ya scouting ni ipi! Scouting wameachiwa mawakala, klabu kazi yake ni kuwa na timu inayofikia malengo yake, otherwise labda uniambie malengo ni kufanya scouting
 
Habari za weekend wakuu,

Ni siku nyingine tena natumai ni wazima wa afya na mnaendelea na majukumu ya kila siku vizuri pamoja na walio mapumnziko.

Wakuu Kuna hili tatizo linalojirudia la huyo kipa anayeitwa (Tanzania one) na hakuna matumaini ya kuisha au kupungua kwani tatizo hili ni la mda mrefu Sana kwa kipa huyu wa club ya SIMBA.

MANULA ni dhaifu sana kwenye mipira iliyokufa (set pieces) na mipira ya mbali ambayo inaonekana Ina mpa shida kwa mda mrefu Sana, udhaifu huo ndio chanzo Cha SIMBA kupoteza michezo ya kimataifa kwa idadi kubwa ya magoli kutokana na tatizo Hilo la mda mrefu linalomtesa kipa huyo.

Jana SIMBA walikuwa na michezo wa ligi kuu dhidi ya MTIMBWA SUGER na kutoka sare ya bao moja kwa moja Ila mazingira ya goli alilofungwa MANULA ni aina ile ile ya magoli anayofungwa kila siku kwa makosa yale ya kutoka golini bila kuangalia movement za mabeki wake.

Hili tatizo ni la defense nzima ya simba kwa ujumla japo MANULA ndo muhanga wa mipira hiyo kwani anakosa, mawasiliano na mabeki Wake, tatizo Kama Hilo lilikuwa lina wasumbua Sana LIVER POOL msimu wa 2017/2018 - japo kuwa wenzetu huwa wana fanya match assessment, na seoson assessment ambapo ni tofauti na kwetu Ila walipunguza tatizo Hilo baada ya kumsajili VIRGIL VAN DIJK msimu ulio fuata na kufanikiwa kupunguza tatizo hilo.

Mlio karibu na kocha wa SIMBA wa makipa mumpe taarifa kwamba CCL zile tano kuna uwezo mkubwa wa kujirudia na zaidi Kama tahadhari zisipo chukuliwa mapema.

By- shabiki wa damu
Pazia hilo.
 
SIMBA ni ile ile na tatizo lile miaka miwili imepita aina ya magoli anayofungwa simba ni ile ile hivi simba wana mechi analyst kweli anayewasaidia kutatua matatizo kwenye timu yao.
 
SIMBA ni ile ile na tatizo lile miaka miwili imepita aina ya magoli anayofungwa simba ni ile ile hivi simba wana mechi analyst kweli anayewasaidia kutatua matatizo kwenye timu yao.
Anafungwa Menddy ije kuwa Manula???
 
Asilimia 80 ya magoli yote anayofungwa Simba hufungisha yeye na Kapombe.
 
Manula haoni mbali ni kama alivyokuwa Mckenzie Ramadhani
 
Back
Top Bottom