Bolivia. Kisa cha Jhonatan Acosta (30) kimewashangaza wengi baada ya kuishi kwa kula minyoo na wadudu kwa zaidi ya siku 30 tangu alivyopotea katika msitu wa Amazon.
Akifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Unitel alisema, "Ilinibidi kujifunza mbinu mpya za kuishi, nilijilazimu kutumia wadudu, kunywa mkojo wangu, kula minyoo na nilishambuliwa na wanyama."
Acosta aliripotiwa kutoweka na familia yake mwishoni mwa Januari, alipokuwa katika shughuli zake za kuwinda na marafiki zake wanne kwenye msitu wa Amazon lakini akajikuta anapotea kwenye eneo hilo lenye kutisha.
Mwezi mmoja baadaye, alipatikana na timu za utafutaji na uokoaji, maafisa walikuwa wanamtumia mbwa aliyepewa mafunzo maalum (Titan) kusaidia kumtafuta Acosta, kituo hicho kiliripoti.
Acosta aliiambia Unitel kuwa mvua ilinyesha nusu ya muda wote aliopotea, alitumia viatu vyake vya mpira kukinga maji ya mvua, lakini mvua zilipoacha kunyesha alianza kunywa mkojo wake mwenyewe. "Nilimwomba sana Mungu mvua," Acosta alisimulia kwa uchungu.
Anasema wakati wa usiku alikuwa aking’atwa na kila aina ya viumbe na wadudu tofauti tofauti.
Dada yake, Miladde Acosta, aliiambia Unitel TV kwamba kaka yake "ilimbidi kupigana na nguruwe, ambaye ni mnyama wa mwituni na hatari zaidi."
Credit: MWANANCHI