Aishitaki hospitali na kudai fidia ya Ksh 6.4 baada ya nesi ambaye ni "Ex wake" kumshona kihuni

Aishitaki hospitali na kudai fidia ya Ksh 6.4 baada ya nesi ambaye ni "Ex wake" kumshona kihuni

Nae alikua na jeuri gani kuhudumiwa na nesi ambae ni x wake? Mi ningesepa labda kama hamna hospital nyingine
 
KIJANA Evans Mutugi ameishitaki Hospitali ya Maura nchini Kenya kwa kitendo cha yeye kufanyia ushonaji usio kuwa wa kibinadamu na nesi ambae anadaiwa kuwa aliwahi kuwa mchumba wake (ex-girlfriend).

Tukio hilo la kustaajabisha lilitokea Jumatatu iliyopita, Novemba 8, 2021 baada ya Mutugi kupelekwa hospitalini hapo kwa matibabu ya dharura baada ya kupata ajali ya pikipiki siku ya Jumamosi, Novemba 6, 2021 majira ya mchana ambapo alipokelewa na kuhudumiwa na nesi huyo aitwaye Rose Kagwira (ex-wake).

Mutugi kupitia wanasheria wake wa John & K company ameishitaki hospitali hiyo na kudai fidia ya kiasi cha Ksh milioni 6.4 sawa na Tsh milioni 131.66.

malunde.com
View attachment 2012394
Wakenya Wana roho mbaya sana.
 
Duh, demu mhuni kweli, amehakikisha msela hang'oi pisi kali tena... Dadeq! 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Huyo jamaa sio kwamba walikula deal na huyo demu wake Ili waipige hospital?Huko Kenya Kila kitu kinawezekana😂😂😂
 
Back
Top Bottom