Elections 2010 AJABU: Kikwete amepata kura nyingi kuliko Dr. Slaa kwenye Jimbo la Mh. Mbowe?

Elections 2010 AJABU: Kikwete amepata kura nyingi kuliko Dr. Slaa kwenye Jimbo la Mh. Mbowe?

Muhimu hapa ni mabadiriko makubwa, wabunge wengi wa CAHDEMA inaonyesha jinsi gani Dr Slaa alivyocheza karata yake vyema, wabunge wengi, ruzuku kubwa kwa CHADEMA, mshahara mkubwa kwa Dr Slaa hata kama aendi bungeni...Hii ndiyo biashara ya siasa, maana inaonekana watu hawajui mchezo huu...:doh:
 
Watu fulani wakifulia hawakosi visingizio,eti yule jamaa katuangalia vibaya ndio maana tumeshindwa!Mijitu mingine bibi!
 
:sad:Matokeo haya ya uchaguzi yananipa picha kuwa level ya elimu kwa Watanzania ni ndogo sana, huwezi chagua kipande cha chupa na kuacha almasi. Kitendo cha CCM kufanya elimu ya msingi kuishia darasa la saba ndio sababu ya kuwa na taifa hili la mambumbumbu...:sad:
 
Nilisema mapema wakati matokeo yanaanza kutangazwa baada ya kuona ktk kituo kimoja Mbowe kapata kura 118 sawa na JK na Mbunge wa CCM kapata 77 na Slaa 75, hata kama JK anapendwa sana haiwezekani akapata exactly figure na mgombea wa upinzani. Kama anapata zote za Chadema na za CCM angepata kura 200 ktk kituo hizo si kubadilishana na Slaa; Hiyo imetokea majimbo mengi sana
 
Kasheshe,

..hii inathibitisha kwamba CCM hawakufanya maandalizi ya kutosha na walikosa umakini ktk uchakachuaji.

..kwanini wasichakachue kule ambako Chadema hawakusimamisha wagombea kabisa?
 
JK amepata kura nyingi kuliko Dr. Slaa kwenye Jimbo la Mh. Mbowe?
Ukistaajabu ya Jimbo la Hai, utaona ya Database ya wapiga kura ya NEC ambapo idadi ya wapiga kura kwa kura za urais inatofautiana kwa kiwango kikubwa na idadi ya wapiga kura kwa kura za ubunge nchi nzima!!!!!!!!!!!
Kulikoni NEC???????
 
Ofcourse hiki kiliwadanganya sana wengi kwa kampeni gani aliyofanya SLAA HAI amshinde JK HAI! wananchi wanajua dk asubiri, ila kwa sababu hana kazi kama mtikila ataandaa nyaraka aende Mahakamani
labda ungesema hana kazi ka maalimu seif haaa haaaaa
 
Hili si jimbo lile, ambalo pamoja na lile la Arusha Mjini, ambalo wakurugenzi wake wa uchaguzi, (yaani ma--Returning officers) walihamishwa ghafla kwani serikali ya CCM iliona walikuwa wanatenda haki? Madhumuni ya transfer hizo ni kuhakikisha CCM inayachukuwa majimbo hayo. Kwa Mbowe waliambulia kuchakachua kura za urais tu.

naan hata arusha hope ni za urais tu walifanikiwa za madiwani na mbunge zilibaki salama chini ya ulinzi shirikishi wa wazalendo wa nchi hii!
 
Nilisema mapema wakati matokeo yanaanza kutangazwa baada ya kuona ktk kituo kimoja Mbowe kapata kura 118 sawa na JK na Mbunge wa CCM kapata 77 na Slaa 75, hata kama JK anapendwa sana haiwezekani akapata exactly figure na mgombea wa upinzani. Kama anapata zote za Chadema na za CCM angepata kura 200 ktk kituo hizo si kubadilishana na Slaa; Hiyo imetokea majimbo mengi sana

Mkuu Halisi,kituo unachozungumzia mimi ndio nilikuwa wakala wa CHADEMA. Tatizo ni kuwa Dr. Slaa hakufanya kampeni zozote za kweli jimboni Hai,alibase zaidi Hai mjini ambako hata bila kampeni angeongoza. Pia wasimamizi wa vituo waliwaelekeza wasiojua kusoma kumchagua jk. Walishindwa kwa Mbowe kwani picha yake ilitosha kumpatia kura.
Uchakachuaji wa jimbo la Hai ulifanyika pale walipowaeka wananchi busy kusubiri matokeo ya ubunge kwa zaidi ya saa 18.
 
Aise acha utani..kituo gani?
 
Back
Top Bottom