Ukistaajabu ya Jimbo la Hai, utaona ya Database ya wapiga kura ya NEC ambapo idadi ya wapiga kura kwa kura za urais inatofautiana kwa kiwango kikubwa na idadi ya wapiga kura kwa kura za ubunge nchi nzima!!!!!!!!!!!JK amepata kura nyingi kuliko Dr. Slaa kwenye Jimbo la Mh. Mbowe?
labda ungesema hana kazi ka maalimu seif haaa haaaaaOfcourse hiki kiliwadanganya sana wengi kwa kampeni gani aliyofanya SLAA HAI amshinde JK HAI! wananchi wanajua dk asubiri, ila kwa sababu hana kazi kama mtikila ataandaa nyaraka aende Mahakamani
Hili si jimbo lile, ambalo pamoja na lile la Arusha Mjini, ambalo wakurugenzi wake wa uchaguzi, (yaani ma--Returning officers) walihamishwa ghafla kwani serikali ya CCM iliona walikuwa wanatenda haki? Madhumuni ya transfer hizo ni kuhakikisha CCM inayachukuwa majimbo hayo. Kwa Mbowe waliambulia kuchakachua kura za urais tu.
Nilisema mapema wakati matokeo yanaanza kutangazwa baada ya kuona ktk kituo kimoja Mbowe kapata kura 118 sawa na JK na Mbunge wa CCM kapata 77 na Slaa 75, hata kama JK anapendwa sana haiwezekani akapata exactly figure na mgombea wa upinzani. Kama anapata zote za Chadema na za CCM angepata kura 200 ktk kituo hizo si kubadilishana na Slaa; Hiyo imetokea majimbo mengi sana
Mkuu Halisi,kituo unachozungumzia mimi ndio nilikuwa wakala wa CHADEMA. Tatizo ni kuwa Dr. Slaa hakufanya kampeni zozote za kweli jimboni Hai,alibase zaidi Hai mjini ambako hata bila kampeni angeongoza. Pia wasimamizi wa vituo waliwaelekeza wasiojua kusoma kumchagua jk. Walishindwa kwa Mbowe kwani picha yake ilitosha kumpatia kura.
Uchakachuaji wa jimbo la Hai ulifanyika pale walipowaeka wananchi busy kusubiri matokeo ya ubunge kwa zaidi ya saa 18.
Aise acha utani..kituo gani?