Down To Earth
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 21,940
- 16,643
#HABARI Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma kwa kutumia basi la Kampuni ya Shabiby namba T 341 EEU, wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuanguka katika eneo la Kihonda Manispaa ya Morogoro na kujeruhi abiria kadhaa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema dereva wa basi hilo alikuwa anamkwepa mwendesha bajaji.
Akizungumzia ajali hiyo Afisa Habari na Mahusiano Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro Betrice Kapoli amesema leo majira ya saa 12 na dakika 45 asubuhi walipokea majeruhi 22 wa ajali ya Shabiby Kati Yao wanaume 5 wanawake 17 ambao wanaendelea kupata matibabu hospitalini hapo.
Credit: #EastAfricaTV