Ajabu: Simba SC itaitoa TP Mazembe kwa Aggregate ya magoli ambayo itawashangaza wengi

Kwa sisi watu wa mpira tunajua soka ina surprise nyingi..lolote lawezekana.
 
Chukua tiket ya platinum siyo diamond ntakuja kulipa!

wakati ukuta.
 
Habari zenu wakuu,

Niende kwenye mada moja kwa moja...bila shaka sote tunafahamu kuwa Kesho (tarehe 06/04/2019) Simba Sports Club ya Tanzania inaanza Kutupa karata yake ya mchezo wake wa kwanza wa robo fainali ya CAF CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya Miamba ya Lubumbashi DRC Tout Puissant Mazembe (Les Englebet) kwenye uwanja wa Taifa (A.K.A Kwa Mkapa).

Mchezo huo ambao umeonekana kuvuta hisia za wapenzi wengi wa soka umekuwa gumzo kila mahali huku watu/mashabiki wengi wa soka wakiipa nafasi kubwa TP Mazembe kuitoa Simba Mashindanoni pamoja na kwamba Simba wanaonekana bora zaidi wakiwa uwanja wa nyumbani, ila watu wengi na hata Benchi la ufundi la TP Mazembe lina imani kuwa Simba hawatatoka salama Kwenye mechi ya marudiano kule Lubumbashi.

Ukweli ni kwamba Simba SC ina uwezo wa kuitoa Mazembe na kuwaduwaza wale wanaoibeza. Simba Sc itawashangaza wengi kwani uwezekano wa kupata matokeo chanya Hapa Dar es Salaam na kule Lubumbashi ni mkubwa.

KWANINI NASEMA HIVI?
Nasema hivi kwa sababu Mpaka kufikia hatua hii hakuna hata mmoja kati yetu aliyeipa Simba nafasi ya 100% ya kufuzu hatua hii ya robo fainali. Baada ya Vichapo Vitakatifu vya goli 5-0 kutoka kwa AS Vita na Al Ahly kwa kila mchezo, kwa hakika watu waliikatia tamaa Simba ila walishindwa kujua target ya Simba ambayo ilikuwa ni kuhakikisha kuwa wanashinda mechi zao zote za nyumbani na kwa hakika lile rundo la magoli kutoka kwa Vita na Al Ahly halikuwa kitu mbele ya point 9 za Simba ilizozipata pale taifa na hatimaye kufuzu na kuwaduwaza Watu wengi Africa.

Hivyo basi, Kwenye hatua hii Strategy ya Simba itabadilika na watahakikisha wapata ushindi Dar na kuhakikisha wanapata matokeo chanya kule Lubumbashi jambo ambalo kwa Simba linawezekana na litafanikiwa kwa asilimia 98%. Nawasilisha.

#Louis (The Second)
#Yes-We-Can
#Mazembe-must-die-by-any-means
#Do-Or-Die
Futuhiiiii ni futuhi
tapatalk_1553855192400.gif
 
Nikiwa kwenye story za soka daima huikumbuka SIMBA nafurahi kuiona timu yangu ikitinga nusufainali
 
Siyo kila wazo linalokuja kwenye ubongo unaliwasili hapa, sijaona sababu ya kimpira uliyoandika
Habari zenu wakuu,

Niende kwenye mada moja kwa moja...bila shaka sote tunafahamu kuwa Kesho (tarehe 06/04/2019) Simba Sports Club ya Tanzania inaanza Kutupa karata yake ya mchezo wake wa kwanza wa robo fainali ya CAF CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya Miamba ya Lubumbashi DRC Tout Puissant Mazembe (Les Englebet) kwenye uwanja wa Taifa (A.K.A Kwa Mkapa).

Mchezo huo ambao umeonekana kuvuta hisia za wapenzi wengi wa soka umekuwa gumzo kila mahali huku watu/mashabiki wengi wa soka wakiipa nafasi kubwa TP Mazembe kuitoa Simba Mashindanoni pamoja na kwamba Simba wanaonekana bora zaidi wakiwa uwanja wa nyumbani, ila watu wengi na hata Benchi la ufundi la TP Mazembe lina imani kuwa Simba hawatatoka salama Kwenye mechi ya marudiano kule Lubumbashi.

Ukweli ni kwamba Simba SC ina uwezo wa kuitoa Mazembe na kuwaduwaza wale wanaoibeza. Simba Sc itawashangaza wengi kwani uwezekano wa kupata matokeo chanya Hapa Dar es Salaam na kule Lubumbashi ni mkubwa.

KWANINI NASEMA HIVI?
Nasema hivi kwa sababu Mpaka kufikia hatua hii hakuna hata mmoja kati yetu aliyeipa Simba nafasi ya 100% ya kufuzu hatua hii ya robo fainali. Baada ya Vichapo Vitakatifu vya goli 5-0 kutoka kwa AS Vita na Al Ahly kwa kila mchezo, kwa hakika watu waliikatia tamaa Simba ila walishindwa kujua target ya Simba ambayo ilikuwa ni kuhakikisha kuwa wanashinda mechi zao zote za nyumbani na kwa hakika lile rundo la magoli kutoka kwa Vita na Al Ahly halikuwa kitu mbele ya point 9 za Simba ilizozipata pale taifa na hatimaye kufuzu na kuwaduwaza Watu wengi Africa.

Hivyo basi, Kwenye hatua hii Strategy ya Simba itabadilika na watahakikisha wapata ushindi Dar na kuhakikisha wanapata matokeo chanya kule Lubumbashi jambo ambalo kwa Simba linawezekana na litafanikiwa kwa asilimia 98%. Nawasilisha.

#Louis (The Second)
#Yes-We-Can
#Mazembe-must-die-by-any-means
#Do-Or-Die

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sisi watu wa mpira tunajua soka ina surprise nyingi..lolote lawezekana.
Ni kweli.....nani aliyekuwa anajua kuwa Ajax wangeitoa Madrid UEFA? In football any result is possible for both teams regardless of their difference in rankings.
 
Back
Top Bottom