AJABU ZA MBEYA NA DAR: Bodaboda, Bajaj, vipanya vs Coaster daladala

AJABU ZA MBEYA NA DAR: Bodaboda, Bajaj, vipanya vs Coaster daladala

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Kwenye hii miji miwili ya MBEYA na DAR ES SALAAM kuna mambo yanachekesha sana. Unajiuliza wafanya maamuzi walikuwa wanatafakari kweli? Mbona walifanya maamuzi ambayo yako Illogical!

Mwaka 2008 Dar es Salaam jiji walipiga marufuku mabasi madogo almaarufu vipanya "Hiace".

Sababu ilikuwa ni usumbufu unaosababishwa na uwingi wa mabasi haya madogo. Ajabu yake wakaruhusu Bajaji ambazo bila kumung'unya maneno kwa sasa zimegeuka kero kubwa sana katikati ya majiji ya Dar es Salaam na Mbeya.

Mbeya miaka kama mitano hivi iliyopita walipiga marufuku "hiace" kubeba abiria katikati ya jiji; ajabu wakaruhusu Pikipiki za magurudumu matatu 'Bajaj' ambazo zimekuwa utitiri na kero kubwa katikati ya jiji la Mbeya.

Mbeya jiji Pikipiki hizi zimekuwa kero kiasi cha kushindwa kuzidhibiti zisiingie katikati ya jiji (Inasemekana majority ni zao hao wafanya maamuzi kiasi kwamba wameshindwa kuamua kuzizuia zisiingie katikati ya mji). Mji umekuwa mchafu sababu ya hizi pikipiki. Hizi zilete raia barabara kuu wadake daladala waingie mjini, zisije town.

Hata ufinyu wa barabara katikati pale Mbeya Bajaj wanachangia pakubwa sana(na wanavurugu sana barabarani); zilitakiwa ziishie njia za kuingia Ituha, Uyole junction, Mama John, Njiapanda ya Veta, Njiapanda ya Isanga nk.

SASA najiuliza what was the logic behind kuzuia Haya mabasi madogo na kuruhusu pikipiki za matairi matatu kwenye both cities? Siasa? au ni nini!!!

Dar es Salaam kwa Mfano...hii Morogoro road Daladala zimekuwa kero kubwa, pamoja na msimamo kwamba kwa sababu kuna mwendokasi basi daladala hizi zingeondolewa...kinachotokea sasa ni kwamba kuanzia Ubungo hadi Fire hakuna vituo vya DalaDala Hawa jamaa wanasimama popote kubeba abiria kwa sababu hii haikuwa plan kuwe na daladala bali mwendo kasi. Wanasimama katikati ya barabara na kusababisha watumiaji wengine wa barabara wakae foleni muda mrefu. Jioni kuna vibajaji vinavyoenda Kimara vinapakia abiria katikati ya barabara kuu hasa mitaa ya Urafiki na Shekilango pale (Unajiuliza Police Usalama barabarani wameshindwa kazi yao kuwaondoa hawa?)

Kama tunaona Mwendokasi hatoshi kuhudumia hii route...basi jengeni Vituo vya daladala kuanzia kimara hadi Fire kuondoa kero kwa watumiaji wengine wa barabara. Sasa hivi ikiwa unatoka Ubungo kuelekea katikati ya mji kupitia Morogoro Road unaweza kutumia masaa hata manne njiani kisa daladala kujenga foleni kwa kupakia abiria njiani(hawana vituo siwalaumu). Tuwe na Option mobile tu Aidha tuwaondoe daladala au tujenge vituo vya daladala, au mwendokasi iongezewe Nguvu zaidi.

TUPUNGUZE KERO HIZI TUOKOE MUDA TUJENGE UCHUMI. TUNAPOTEZA SANA MUDA NJIANI NA KUZOROTESHA UCHUMI WETU BILA SABABU ZA MAANA.

WANAMAAMUZI WAJIBIKENI KWENYE HAYA MAJIJI YA MBEYA NA DAR ES SALAAM
cover-pic.jpeg
D2AtWN_XgAACrue.jpeg
 
Nenda Arusha barabara ya chini ya mti/idara ya maji, njoo stand kuu, pita friends corner kwenda soko la samunge, tembea Sokoine road pita Kilombero market kwenda Corner ya Nairobi ni uchafu mtupu wa Bajaj. Dereva wa Bajaj hawana nidham U turn ni popote, parking ni popote abiria anabebwa popote na hakuna kiongozi wala police anakohoa kwenye hili.

Hili nalo wakalitazame.
 
Nenda Arusha barabara ya chini ya mti/idara ya maji, njoo stand kuu, pita friends corner kwenda soko la samunge, tembea Sokoine road pita Kilombero market kwenda Corner ya Nairobi ni uchafu mtupu wa Bajaj. Dereva wa Bajaj hawana nidham U turn ni popote, parking ni popote abiria anabebwa popote na hakuna kiongozi wala police anakohoa kwenye hili.

Hili nalo wakalitazame.
Ni tatizo kubwa hasa pale Halimashauri za haya majiji zinapoonekana kushindwa kazi kudhibiti hizi pikipiki. Huduma zam wananchi wanazihitaji sawa, lakini sio waingie katikati ya miji. Watoe huduma kwenye feeder roads huko. Barabara Kuu na za mijini zitumiwe na magari tu.

Nashangaa kamba kama Malori wameweza kuyazuia kwanini vibajaji viwe kero!!!
 
Mbeya ni sehemu moja stressfull kuwepo hasa ukiwa maeneo ya mjini. Bajaji nywiii nywiii nywiii here and there... kelele barabarani halafu barabara yenyewe nyembamba. Bajaji zenyewe zimekongoroka kama zinataka kumwagika . 😅

Bora Dar, barabara ni nyingi na pana kiasi.

WaTz hivi hatuwezi kufanya kitu chochote kwa usahihi.

Sorry not sorry.
 
Back
Top Bottom