Waarabu nao ni watanzania pia kwasababu walizaliwa hapahapa, hawindi pia, pamoja na kwamba wazazi wao zamani walitokea bara lingine au nchi nyingine, lakini ni watazania, hawana kwa kwenda, hapa ndo kwao. vivyohivyo, hata hapa tz, kuna makabila mengi tu ambao ni wahamiaji, kuna kabila la wangoni ambao walitoka south africa, wapangwa vile vile walitoka south africa. si unakumbuka mfecane war?, pia kuna watz wengi sana hapa ambao walitokeaga congo, mozambique,malawi na zambia. hii Tanzania ukichunguza, ni ya watu wachache sana, hawawezi kujaa hata mkoa mmoja kama wakikusanyika, wengi wetu ni wakuhamia tu, mababu zetu walihamia. pamoja na kwamba sisi ni weusi, tusijifanye kuwa ni wamiliki pekee wa hii ardhi ambayo Mungu aliiumba kwa watu wote. mimi ni mweusi, ila sioni kama ni busara kuongea kama waarabu sio wakwetu. Upendo ni muhimu sana ktk jamii yetu, tudumishe upendo tuondoe ubaguzi. kuna waswahili wengi tu wanawavamia na kuwaua waarabu hapa bongo, kwa ujambazi au hata ugomvi, lakini hilo huwa haliandikwi au kuchukuliwa kama ni kubwa. racism is not good. Tanzania sio nchi teule ambayo watu walipewa na Mungu kama nchi zingine zilivyo, hata hii mipaka iliwekwa na watu tu toka ulaya, zamani haikuwapo Tanzania hii. racism is sin, because it lucks love in it.