Ajali iliyoua watu 6 Dodoma: Wanaopaswa kukamatwa na kuwekwa ndani ni Mfugale na Meneja wa Dodoma wa TANROADS Dodoma, sio dereva wa lori

Mkuu inawezekana hakuna sheria ya kuwashutaki Tanroads kama msimamizi wa hiyo barabara though anatakiwa kuwa responsible hata bila mahakama.
Inawezekana sheria ya manunuzi inawabana Tanroads ku act immediately kwenye issues za minor repairs kama hizo. Kunauwezekana mkubwa Tanroads Dodoma wako kwenye process za ku attend hiyo dharura kwa kutumia sheria ya manunuzi ambayo hairuhusu ku process na kuanza kazi within hours. Kama sheria ya manunuzi ni kikwazo bora iwe amended ili kupunguza ama kumaliza kabisa madhara kama hayo.

Tanroads hawakwepi lawama kwani walitakiwa waweke alama za tahadhari kuanzia 100m kabla ya eneo usika. Wabgeliweka pamoja na alama zingine hata hata bumps za mchanga ili kulazimisha madereva wazembe wapunguze mwendo na hatimae kuepusha ajali kama hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kulikuwa na alama kwenye hilo shimo?
 
Tanroads ni wazembe sana, kutoka Makambako kwenda Mbeya kuna kipande fulani cha barabara pale katikati kinaweza kukutoa roho kwa mashimo yaliyopo.
Labda kutokea igawa kwenda mbeya na si makambako?
 
Labda kutokea igawa kwenda mbeya na si makambako?
Yes itakua kuanzia igawa, ukitoka makamboko kuna barabara mpya, ukiimaliza tu hiyo ni majanga matupu.
 
Hata barabara za mijini watu mnavyokepana kwenye mashimo ni balaa, sijwahi kukutana na gari inayofanya ukaguzi wa barabara. Hizi barabara zitakuwa zinakaguliwa hapo ofisini kwenye kompyuta, mithili ya mtu anayeangalia kideo
Huku Dar mateja wanafukia mashimo kiaina then wanawatoza ushuru wenye magari yanayopita hapo.
 
Dereva wa lori wamstaki kwa kuua !

Kwanini hakuingia kwenye hilo shimo badala yake akaamua kugonga coaster basi lenye abiria?

Huyo wazae nae iwe fundisho kwa madereva wote wanaoua watu na kuwasababishia ulemavu wa kudumu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANROAD NI SAWA NA JIPU LA MATTAKO KUKAA KU CHUNGU.KULALA CHALI KIVUMBI[emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2088]nduki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku Dar mateja wanafukia mashimo kiaina then wanawatoza ushuru wenye magari yanayopita hapo.
Katika hali ya kawaida huwezi kutarajia kukutana na shimo kwenye barabara ya lami, na hata kuweka matuta kwenye barabara za lami ni upuuzi wa hali ya juu sababu ni rahisi kusababisha ajali kama dereva hakutarajia kukutana na hilo tuta na yupo speed zaidi ya 80, haya mambo yapo Afrika tu kwenye ngozi nyeusi..yaani dereva unakuwa umejiandaa kisaikolojia kukwepa mashimo na kuruka bumps...which means safari ya masaa 2 itabidi utumie masaa hadi 10 sababu itabidi uendeshe mwendo wa kinyonga kujitahadhari na mashimo ya hapa na pale na zile bumps za ghafla bin vuuu zisizokuwa hata na alama yoyote, na inakuwa hatari zaidi kwa wale madereva ambao hawatumii hiyo barabara mara kwa mara..
 
Sehemu kubwa ya barabara zetu si zakuendesha zaidi ya 60km/h kulingana na design yake na associated risks kama vile kupishana uso kwa uso kwenye high ways.

Wanaweka matuta kama njia mojawapo ya kukabiriana na hizo associated risks otherwise hali ingelikuwa mbaya sana.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni shida sana, kuna barabara ya lami imejengwa goba-makongo imejazwa matuta hadi unashangaa, kila mita 100 unaruka tuta. Yaani unajenga barabara nzuri ya lami unaishia kuiharibu na matuta. Unaishia kusababisha usumbufu kwa madereva na kuwaingiza gharama za matengenezo ya shock up na gharama za mafuta. maana utaendesha hapa na hapa unapunguza mwendo kuruka tuta
 
Ukiendesha gari ndiyo utajuwa kile ambacho mtoa mada anaongea hiyo barabara nimepita jumapili nikitokea Mwanza nikiwa na gari ndogo hakika tanroads wanahitaji kufanya kazi za ziada juu ya barabara.
Kuna vipande unapita unaweza ukafikiri upo shambani
 
Ukiendesha gari ndiyo utajuwa kile ambacho mtoa mada anaongea hiyo barabara nimepita jumapili nikitokea Mwanza nikiwa na gari ndogo hakika tanroads wanahitaji kufanya kazi za ziada juu ya barabara.
Kuna vipande unapita unaweza ukafikiri upo shambani


Hata Wafanyakazi wa AZAM TV pale Kizonzo - Shelui walikufa kwa ajali ya Lorry na Coaster kwa pamoja wakikwepa mashimo katikati ya barabara,

Ajabu Tanroad hawakuguswa.
 
Tanroad wazembe sanaaaaa, barabara ya kusini mbagala, vikindu,mkulanga, kibiti Ni mbovu haswa yaani mashimo mengi Sana hasa eneo la kisemvule pale daaah Ni hatariii Sana,

Pale Kisemvule mashimo mengi Sana Tanroad mkoa wa Pwani acheni kukaa ofisini mje mfanyie marekebisho haya!!

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
Naungana na mtuma post,mashimo ya barabarani ni moja ya sababu kubwa ya ajali,2011 tulipata ajali Mbalamaziwa jirani na Makambako,sababu ni mashimo,2015 Ikungi Singida ajali nyingine iliondoka na roho ya dereva wa costa akakutana uso kwa uso na basi kisa kukwepa shimo kubwa,hawa TANROADS ifikie kipindi wachukuliwe hatua ajali kama hizi zinapotokea wasiangaliwe madereva tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…