Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
WakuuAjali mbaya imetokea asubuhi ya leo katika eneo la Mombasa, Ukonga, ambapo lori la mkaa kama unavyoona kwenye picha limegonga gari dogo aina ya IST kwa nyuma.
Dereva wa gari aina ya IST aliposikia honi hizo na kuona lori likija kwa kasi, alijaribu kujinusuru kwa kuongeza mwendo, lakini kwa bahati mbaya alijikuta akigonga daladala iliyokuwa mbele yake.
Wakati hayo yakitokea, dereva wa Bajaj naye alikuwa akipenya katikati ya magari akitafuta nafasi ya kuwahi, akaingia katikati ya gari dogo na lori lililofeli breki, akagongwa vibaya na kusababisha Bajaj yake kuharibika vibaya.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa kuna hofu ya vifo kutokana na ajali hiyo, ingawa idadi kamili ya waathiriwa bado haijathibitishwa. Tusubiri Vyombo vya usalama vitatoa taarifa kuhusu tukio la ajali hii.