Ajali mbaya ya treni

Ajali mbaya ya treni

Military Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2019
Posts
761
Reaction score
1,464
IMG-20200409-WA0029.jpg


images.jpg


Ilikuwa ni ijumaa ya September 12, 2008 jioni ya saa kumi UTC ambapo ilitokea ajali mbaya ya treni ya Metrolink 111 mjini Chartworth, California US iliyosababisha vifo vya watu 25 na majeruhi zaidi ya 135.

Mmoja kati ya watu waliofariki katika ajali hiyo alikuwa ni Charles Peck mwanaume wa umri wa miaka 49 aliyefariki pamoja na mkewe na watoto wao wawili wakubwa, ajabu ni kuwa mwili wa Charles haukupatikana mapema kama ilivyokuwa kwa miili mingine.

Utafutaji wa mwili wake ulitegemea zaidi katika kufuatilia mawasiliano yake 35 ya simu alizopiga na kupigiwa baada ya ajali kutokea, kufuatia kuonekana kwa kuingia na kutoka kwa simu hizi, ikaaminika kuwa Charles hakua amefariki, angepiga vipi simu na kupokea kama angekua amefariki?

Licha ya simu hizo zote ambazo nyingi zilikuwa zikipigwa na watu wa familia yake, lakini katu hawakuwa wakisikia sauti ya Charles, baada ya simu kupokelewa walikuwa wakisikia tuu sauti ambazo hawakuweza kuzielezea ni sauti za aina gani, bado wakaamini kuwa Charles yuko hai, na ndiye anapokea simu hizo.

Masaa 12 baada ya ajali kutokea Charles alipatikana, alikuwa amefariki masaa 12 nyuma tangu ajali ilipotokea, lakini ajabu ni kuwa simu yake ilikutwa ikiwa imefanya mawasiliano lisaa limoja tuu lililopita, na simu hio ndio iliyofuatiliwa hadi kupatikana kwa mwili wa Charles.

Mpaka leo wachunguzi hawakuwahi kutangaza zaidi juu ya nini kilikuwa kinafanya mawasiliano na watu kupitia simu ya Charles aliyokutwa nayo wakati yeyye alikuwa amefariki muda huo huo ajali imetokea.

IMG-20200409-WA0028.jpg


@military_Genius
 
Back
Top Bottom