Ajali Morogoro, watu kadhaa wabanwa na gari la mizigo

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Watu kadhaa wamebanwa ndani ya gari ndogo aina ya costa baada ya gari kubwa la mizigo kuliangukia gari hilo

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Nanenane Morogoro, Polisi wanaendelea kuokoa walioathiriwa na ajali hiyo.

​

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa jumla ya watu 10 wamejeruhiwa huku 4 kati yao wakijeruhiwa vibaya, baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kukandamizwa na Kontena ambalo lilikuwa limebeba Tumbaku katika eneo la Nanenane mkoani humo hii leo.

Kamanda Mutafungwa amesema kuwa ajali hiyo imetokea hii leo Agosti 17, 2020 majira ya saa 3:00 asubuhi, ambapo gari aina ya Costa ilikuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro na ndipo ilipolivagaa Lori hilo ambalo lilikuwa limepata hitilafu iliyopelekea Tela lake kukatika na hivyo kuziba njia yote.


"Tela hilo lilikatika hivyo kusababisha Tela lililokuwa limebeba tumbaku kukata barabara yote na ndipo gari aina ya Costa iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam iliweza kuingia ubavuni kabisa mwa hilo Tela, tumeokoa jumla ya watu 6 wamepelekwa Hospitali na hali zao ni nzuri, lakini pia tumetoa watu 4 ambao walikuwa mbele kabisa na walikuwa wamekandamizwa na hali zao ni mbaya" amesema Kamanda Mutafungwa.

Aidha Kamanda Mutafungwa amesema kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu.

=====

#UPDATES:

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 6 kujeruhiwa baada ya lori kuliangukia basi dogo aina ya Coaster katika eneo la Nanenane mkoani Morogoro.

Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Ritha Lyamuya amethibitisha .
​
 
Pole kwa wahanga..kimvua mvua kimeleta kizaizai..

Everyday is Saturday..........................😎
 
Ifike pahala madereva watumie vizuri sheria zilizowekwa kwa ajili ya usalama wao, abiria, vyombo vyao pamoja na miundombinu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…