Ajali-msaada wa sheria

georgeallen

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
4,118
Reaction score
1,875
Mimi nilikuwa abiria kwenye basi lililopata ajali Mikumi, Morogoro, 2011.
Nilipata majeraha makubwa na kulazwa hospitali kwa miaka miwili-na bado nipo hospitali.
Wakati ndugu wanafuatilia nyaraka za ajali ili kupeleka madai ya malipo bima wamegundua kwamba basi lile lilikuwa na bima ndogo-third party.


Swali

1. Nianzie wapi kufuatilia madai yangu kama gari lilikwa na bima ndogo?
2. Ni nani hapa anawajibika kunilipia gharama za matibabu na kupoteza kipato?
3. Je, kisheria basi za abiria wanaruhusiwa kukata Third party insurance?
4. kama Mmiliki wa basi amegoma kunisaidia gharama za matibabu nifanyeje?
 
1.anza na mwenye gar kwa kumuandikia barua called intention to sue ukidai akulipe akishindwa unamsue.2.mwenye gar ndo atalipia gharama ila ktka kaz utamuomba akulipe kitu kinaitwa prospective damage( tegemeo la badae kulingana na kipato ulichokua unspata; inahitaj hesabu kdgo)kma huwez kurud kazin tena coz of hyo ajali.3.ndio nilazima.4.utafungua kesi mahakaman ili akulipe.kma huwez kufka mahakaman coz ya huo ugonjwa utawkilishwa na ndugu,mzazi,mlezi.au wakili.
 
Hata kama mmiliki wa gari ana bima ndogo bina inasahili kukulipa kutokana na Pollicy zao za passenger liability, kaha hayo malipo hutaridhika nayo unaweza kumhusisha mmiliki wa gari.

Tuwasiliane naweza kukusaidia zaidi.
 

Kwa kuongezea kidogo, bima sio ndogo- ndio maana ya third party! mwenye gari hatalipwa, bima hii ina-cover wewe (maana ya third party) Hivyo asiwe na wasiwasi na third party!
 
mzee, shukurani sana kwa msaada wako. Angalau nimepata pa kuanzia.
 
Hata kama mmiliki wa gari ana bima ndogo bina inasahili kukulipa kutokana na Pollicy zao za passenger liability, kaha hayo malipo hutaridhika nayo unaweza kumhusisha mmiliki wa gari.

Tuwasiliane naweza kukusaidia zaidi.
Asante sana kwa ushauri mzuri. Jumanne nawafuata bima kusikia kauli yao. nitakujulisha kwa ushauri zaidi. asante.
 
Kwa kuongezea kidogo, bima sio ndogo- ndio maana ya third party! mwenye gari hatalipwa, bima hii ina-cover wewe (maana ya third party) Hivyo asiwe na wasiwasi na third party!
Asante sana kwa mchango wako, mkuu. Natarajia kuwaona bima jumanne ijayo, hivyo nitakujulisha maendeleo na kuomba ushauri zaidi. Asante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…