Ajali ni nyingi kati ya Dar to Morogoro na hadi Dodoma

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Mara nyingi nasafiri kwa njia hii na hukutana ajali si chini ya mbili.

Athari za ajali zinafahamika; ulemavu, kupoteza maisha na mali.

Njia hii imekuwa ndogo na msongamano ni mkubwa.

Kama serikali iliweza kutoa ruzuku ya bil 100 kila mwezi, kwanini isitenge bil 30 tu kila mwezi kwa njia hii
 
Tayari tenda zimeshatangazwa na upembuzi yakinifu unaendelea.. Most likely mwakani ujenzi unaanza
 
Hawa watu ilibidi wafike Moro. Ajali ni nyingi na muda unapotea sana njiani.
Iko siku nimefika Maseyu saa kumi jioni Msamvu roudabout saa saba za usiku.☹

Lori moja kutoka Mafinga limeanguka na kusababisha Jamu inayofanana na kisimamo cha kiama.

Na hilo ni tukio moja tu out of maelfu.
 
Mnahitaji barabara pana na njia za kwenda na kurudi Dual carriageway ila pia madereva wanahitaji mafunzo na kuwa professional drivers na la mwisho kila mwenye gari afanye matengenezo mara kwa mara

Unakuta gari linaenda handbrake ilikatika siku nyingi, brake zimeisha kabisa na matairi ndio usiseme yaani mtu anaendesha Bus au Lorry au gari matairi kipara kabisa mpaka waya unaziona

Anasimamishwa na police barabarani anahonga 30,000 anaambiwa nenda

Hiyo nenda ni kama anamwambia kawauwe maadam 10 zangu nazipata mkafe tu

Inatakiwa watu wenye majukumu ya kazi na kufuata sheria sio unajali hizo laki mbili kwa siku unajiona mjanja na kuuwa watu kisa hana brake na unamruhusu aende

Naona kuhusu services za magari ni muhimu ingawa wengi wenye magari wanaunga unga tu maisha ana gari ila kulimaintain hawezi
 
Treni ya mwendo kasi ilikua ni suluhisho kubwa kati ya dar Morogoro hadi Dodoma
 
Treni uwekezaji wake utatumia muda mrefu na hauwezi kuwa mbadala kwa njia mchepuko. Mtu anaenda Kilosa vijijini, Ludewa nk.
Barabara ni muhum mno, tuikabe serikali. Ajali ni nyingi na mara zote makosa huwa eti ya madereva na sio miundombinu
 
Naona kuhusu services za magari ni muhimu ingawa wengi wenye magari wanaunga unga tu maisha ana gari ila kulimaintain hawezi
Pamoja na ubovu na kiwango duni cha barabara zetu, ili nalo ni la msingi.
Kuna vinchi kama Rwanda, angalau uwa wanafanya ile 'roadworthy test' kila mwaka nafikiri.
Au tunaweza kufanya kama UK, ile MOT test ili watu wawe serious na ku service magari yao.
Ingawa Bongo miyeyusho sana; yaani hakuna kitu ambacho kimekaa sawa.
 
Tren haiwezi kuwa muhimu? Kweli wajinga mpo wengi
Treni uwekezaji wake utatumia muda mrefu na hauwezi kuwa mbadala kwa njia mchepuko. Mtu anaenda Kilosa vijijini, Ludewa nk.
Barabara ni muhum mno, tuikabe serikali. Ajali ni nyingi na mara zote makosa huwa eti ya madereva na sio miundombinu
 
Mara nyingi nasafiri kwa njia hii na hukutana ajali si chini ya mbili.

Athari za ajali zinafahamika; ulemavu, kupoteza maisha na mali.

Njia hii imekuwa ndogo na msongamano ni mkubwa.

Kama serikali iliweza kutoa ruzuku ya bil 100 kila mwezi, kwanini isitenge bil 30 tu kila mwezi kwa njia hii
Umesahau tuko awamu ya 6 mkuu
 
Hapo panataka Dual carriageway.
Vinyamkera pia ni vingi njia hiyo
20221112_034722.jpg
 
Back
Top Bottom