ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Hii ni ajali iliyosababishwa kutokana na uzembe wa dereva wa Mwakyembe.
Hivi unajua siku hizi ukimpa Traffic 30,000/= anakuletea Leseni Class C nyumbani kwako jioni hiyo hiyo.!!! Matokeo yake ndio haya, hata common sense ya kuovateki lori inakosekana.
ZeMarcopolo,Mwakyembe apparently alimwambia dereva wake aovertake kwa speed ya 140Km/h, kwahiyo nadhani wenye makosa si madereva peke yao.
Mwakyembe afunguliwe trafic case kwa kumlazimisha dereva wake kuendesha 140km/ph, hii ni overspeed case.
Kesi fiunguliwe bila kuja cheo, pesa kabila. Law is law regardless.
Mwakyembe afunguliwe trafic case kwa kumlazimisha dereva wake kuendesha 140km/ph, hii ni overspeed case.
Kesi fiunguliwe bila kuja cheo, pesa kabila. Law is law regardless.
Kweli TZ hatuko makini kabisa, ile barabara ya Mbeya - Iringa unaweza kuendesha kwa speed ya zaidi ya 140km/h? Hizo ni karibu 90 miles/h kwa UK ambayo ni overspeeding ya 20miles zaidi ya maximum speed kwa motor ways za UK.
Huyu mungu tunamweka kwenye majaribio kweli kweli wakati uzembe ni wetu wenyewe. Kwa ile barabara hata speed ya 100kms/h bado haifai na ukigonga mnyama au binadamu gari litatupwa nje tu.
Ingelikuwa nchi za wenzetu, kwa huo mwendo ambao wamekiri walikuwa wanaenda, huyo dereva angenyang'anywa leseni hapo hapo na kufungiwa kuendesha kwa zaidi ya mwaka mmoja na faini juu. Lakini kwasisi Waafrika tutaishia kusema kuna mkono wa mtu.
Kwa sababu hukuwepo kwenye tukio unaweza kucomment unavyotaka. Ila mimi najua kuwa kulikuwa na khali iliyosababisha afanye hivyo na ameisema wazi kwa vyombo vya habari. Kuepuka kifo unaweza hata kuensedha speed 800kms/h kama gari yako ina uwezo kifo siyo mchezo na dereve alikuwa analeta mchezo mbaya.
Anyway unaweza sema unalotaka na samweli na sikonge watakuja siyo muda mrefu ili muendeleze chuki zenu
Ile barabara pamoja na mambo yote, mara ya mwisho kupita katika barabara hiyo gari nililopanda lilikuwa linakwenda 160-180 km/h. Hii ni kutoka Mbeya -Morogoro. Moro - Dar jamaa alislow down akawa kati ya 120-140km/hKweli TZ hatuko makini kabisa, ile barabara ya Mbeya - Iringa unaweza kuendesha kwa speed ya zaidi ya 140km/h? Hizo ni karibu 90 miles/h kwa UK ambayo ni overspeeding ya 20miles zaidi ya maximum speed kwa motor ways za UK.
Engineer punguza speculations usizokuwa na uhakika nazo.Zinapunguza reliability yako kwa mtu anayeita Engineer(proffession ya mambo hakika)FMES,
Kitu ambacho labda waandishi wetu pamoja na polisi wameshindwa kufanya uchunguzi, ni je ni kweli Mwakyembe alilala Makambako? Kama alilala makambako waliondoka hapo saa ngapi? Kutoka Makambako mpaka Ifunda kisheria ni masaa sio chini ya matatu, kama walifika Ifunda kwenye saa moja, kuna mawili, waliondoka mapema sana au walikuwa wanakimbia sana.
Pia inasemekana waliondoka Kyela saa mbili usiku; kutoka Kyela mpaka Makambako ni kama masaa matano kama unafuata sheria za barabarani. Sasa kama ni kweli ina maana walifika Makambako masaa ya saa saba, watafute guest na kulala na kuondoka kama saa kumi asubuhi, je ina make sense?
Kitu kingine ambacho inatakiwa kujua mnapochangia hili jambo ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake. Kwenye mikutano yake mingi hudiriki hata kusema kuna watu wamejaribu kumpa mamilioni huyo dereva ili amwue lakini dereva siku zote anakataa. Huwa najiuliza kama kuna hayo mambo kwanini hawaendi polisi? Labda ni maneno ya kisiasa zaidi kuliko ukweli. Kilicho ukweli ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake na ningetegemea kabisa afanye lolote lile kujaribu kumwokoa asiingie matatizoni.