Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Hivi unajua siku hizi ukimpa Traffic 30,000/= anakuletea Leseni Class C nyumbani kwako jioni hiyo hiyo.!!! Matokeo yake ndio haya, hata common sense ya kuovateki lori inakosekana.

Yebo yebo,

Nimecheka hiyo comment yako kuhusu common sense ya ku overtake. Hilo swali lipo sana kwenye mitihani ya udereva hasa huku Europe sijui kwa TZ. Wanauliza kitu kama barabara husika maximum speed ni 60m/h, mbele yako kuna gari linaenda speed ya 60m/h na wewe unataka kulipita utafanyeje? Jibu moja wapo ni kwamba utaongeza speed zaidi ya 60m/h ili uweze kulipita haraka. Inaelekea hilo ndilo lingelikuwa jibu pia la dereva wa Mwakyembe. Of course angelikuwa amechemsha.

Tatizo la TZ hata ukiwa dereva mzuri bado unaweza kuja kugongwa au kusababishiwa ajali na hawa madereva fake wa kuletewa leseni nyumbani.
 
Mwakyembe apparently alimwambia dereva wake aovertake kwa speed ya 140Km/h, kwahiyo nadhani wenye makosa si madereva peke yao.
ZeMarcopolo,

Kwa sheria za barabarani, dereva hutakiwa kuchukua amri toka kwa mtu yeyote; amri au agizo ambalo linaweza kusababisha ajali barabarani unatakiwa kulipuuza. Of course kwa Tanzania usipomsikiliza boss uko hatarini kupoteza kibarua chako.

Nawaonea huruma hao madereva wa viongozi
 
Mwakyembe afunguliwe traffic case, ajali hii kajisababishia mwenyewe ndo maana amekubali kua hkuna mtu mwingine involved, Kamlazimisha driver wake ku-overspeed as result ikasababisha hiyo ajali, sisi wote tunaelewa mabosi wa kibongo sipowasikiliza umemwaga unga


Mwakyembe kafanya makosa, no body should be above the law, Mwakiemebe aonyeshe mfano
 
Mwakyembe afunguliwe trafic case kwa kumlazimisha dereva wake kuendesha 140km/ph, hii ni overspeed case.

Kesi fiunguliwe bila kuja cheo, pesa kabila. Law is law regardless.
 
Mwakyembe afunguliwe trafic case kwa kumlazimisha dereva wake kuendesha 140km/ph, hii ni overspeed case.

Kesi fiunguliwe bila kuja cheo, pesa kabila. Law is law regardless.

Bull,

Inaonekana you are too naive in traffic matter as you are with the driving / speeding / overtaking matters are concerned

Mwakembe hawezi kufungulia traffic case kwa vyovyote vile kwa kuwa hakuwa anaendesha gari. Na dreva napaswa kuendesha gari kwa kutumia maamuzi yako na ya si abiria.

We umezoea kendeshea mjini nini?
 
Mwakyembe afunguliwe trafic case kwa kumlazimisha dereva wake kuendesha 140km/ph, hii ni overspeed case.

Kesi fiunguliwe bila kuja cheo, pesa kabila. Law is law regardless.

Duh, wewe una lako jambo mbona unazungumzia vitu ambavyo havipo? Au polisi wametoa kauli kuwa mwendo wake ulikuwa 140 km/ph? NAdhani kama walikuwepo na kumulika kasi ya gari hilo bila shaka wamemkamata na dreva wa lori pia!
 
Mwakyembe speaks on ITV

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=ZoVSS9qh4kU]YouTube - Kulikoni ajali ya Dr. Mwakyembe[/ame]
 
Mwakyembe speaks on ITV

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=ZoVSS9qh4kU]YouTube - Kulikoni ajali ya Dr. Mwakyembe[/ame]
 
Kweli TZ hatuko makini kabisa, ile barabara ya Mbeya - Iringa unaweza kuendesha kwa speed ya zaidi ya 140km/h? Hizo ni karibu 90 miles/h kwa UK ambayo ni overspeeding ya 20miles zaidi ya maximum speed kwa motor ways za UK.

Huyu mungu tunamweka kwenye majaribio kweli kweli wakati uzembe ni wetu wenyewe. Kwa ile barabara hata speed ya 100kms/h bado haifai na ukigonga mnyama au binadamu gari litatupwa nje tu.

Ingelikuwa nchi za wenzetu, kwa huo mwendo ambao wamekiri walikuwa wanaenda, huyo dereva angenyang'anywa leseni hapo hapo na kufungiwa kuendesha kwa zaidi ya mwaka mmoja na faini juu. Lakini kwasisi Waafrika tutaishia kusema kuna mkono wa mtu.

Kwa sababu hukuwepo kwenye tukio unaweza kucomment unavyotaka. Ila mimi najua kuwa kulikuwa na khali iliyosababisha afanye hivyo na ameisema wazi kwa vyombo vya habari. Kuepuka kifo unaweza hata kuensedha speed 800kms/h kama gari yako ina uwezo kifo siyo mchezo na dereve alikuwa analeta mchezo mbaya.

Anyway unaweza sema unalotaka na samweli na sikonge watakuja siyo muda mrefu ili muendeleze chuki zenu
 
Mwakyembe aongea

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=ZoVSS9qh4kU]YouTube - Kulikoni ajali ya Dr. Mwakyembe[/ame]
 
Kwa sababu hukuwepo kwenye tukio unaweza kucomment unavyotaka. Ila mimi najua kuwa kulikuwa na khali iliyosababisha afanye hivyo na ameisema wazi kwa vyombo vya habari. Kuepuka kifo unaweza hata kuensedha speed 800kms/h kama gari yako ina uwezo kifo siyo mchezo na dereve alikuwa analeta mchezo mbaya.

Anyway unaweza sema unalotaka na samweli na sikonge watakuja siyo muda mrefu ili muendeleze chuki zenu

Kwi kwi kwi!!!! kama hiyo ni chuki basi kazi kweli kweli.

Labda wewe ndio una chuki na hao uliowataja na hutaki wachangie jambo lolote la Mwakyembe.

Utakuwa unajisumbua bure maana kila mtu ana haki ya kuchangia na watu kama nyie ambao mungetaka watu wasiandike kitu hamtukoseshi usingizi hata kidogo. Kama hukubaliani na nilichoandika basi njoo na hoja zako na sio kuja na mambo ya kike oohh! chuki na ujinga mwingine.

Inaelekea hata hujui sheria za usalama barabarani zinasema nini na hata kubishana na wewe ni kupoteza muda.
 
remember the accident of Zimbabwe prime minister? na wasiwasi sana na haya malori matupu...
 
Kweli TZ hatuko makini kabisa, ile barabara ya Mbeya - Iringa unaweza kuendesha kwa speed ya zaidi ya 140km/h? Hizo ni karibu 90 miles/h kwa UK ambayo ni overspeeding ya 20miles zaidi ya maximum speed kwa motor ways za UK.
Ile barabara pamoja na mambo yote, mara ya mwisho kupita katika barabara hiyo gari nililopanda lilikuwa linakwenda 160-180 km/h. Hii ni kutoka Mbeya -Morogoro. Moro - Dar jamaa alislow down akawa kati ya 120-140km/h
 
Jamani kuweni wakweli na hawa waandishi wa habari tanzania.. sisi sote tumeishi Bongo na tunajua barabara hizo ziko vipi.. Hakuna Lori la mizigo linalo kwenda mwendo wa 120 au 130Km/hr barabara ya Iringa hasa sehemu iliyotajwa kutokea ajali..
Nikiwa na maana kwamba haiwezekani Dreva wa Mwakyembe alilazimika kuendesha gari 140 Km/hr ili ku overtake lori ambalo lilikuwa likienda mwendo wa kawaida... Na kama kweli gari la Mwakyembe lilikuwa likienda kasi ya 140 km na lingekongwa na lori kidogo tu ubavuni basi lingeangukia over 100 metres from the scene of accident..haikutokea hivyo!..
Hapa maneno yameongezwa - WHY hilo ndio swali la kujiuliza!
 
Mkuu Mkandara,

Wakati mwingine waandishi wa habari wanasaidia kukuza majungu kwa kushindwa kuuliza maswali magumu magumu au kufuatilia habari.

Wengi hapa mmesoma physics, jiulize kama hilo gari lingegongwa kwa nyuma upande wa taa ya kushoto, je lingeangukia wapi? Lingegeuka nyuma upande wa kushoto badala ya kwenda mbele na ingelikuwa ajali mbaya zaidi. Lingegongwa nyuma katikati ndio lingeweza kwenda mbele lakini kwa kuangalia picha hakuna dalili lile gari liligongwa nyuma katikati.

Kwa jinsi nilivyoliona lile gari nina wasiwasi mkubwa sana kwamba liligongwa kwa nyuma. Kugongwa kwa nyuma na lori linaloenda 100km/h, gari lisingelikuwa vile. Pia nina wasiwasi kama lori lenye trela lilikuwa linaenda 130km/h kwenye ile njia ambayo mwendo unaoruhusiwa ni 80km/h.

Labda tukubali tu kuna siasa zimeingizwa na tuendelee mbele kama ambavyo inatokea mara nyingi kwenye mambo ya wakubwa. Inasikitisha sana tunaingiza siasa kwenye kila kitu.
 
labda dereva wa lori ajitokeze na kueleza upande wake
wa hali ilivyokuwa.
 
Mtanzania,
Habari za kudhibitisha tukio hilo toka kwa dereva na Mwakyembe zimethibitisha kwamba lori liliwagonga ubavuni.. Mkuu nimeisha endesha malori makubwa na hata gari ndogo pembeni mwa malori na najua fika kama likikugonga hata kidogo tu utakapo ishia inategemea na kasi ya gari lako...Ni hatari tupu kugongwa na haya malori.
Na kama kweli gari la Mwakyembe lilisimamishwa na mti basi ile kasi inayodaiwa ni uongo mkubwa..Hilo gari la Mwakyembe lisingekuwa hivyo kama tulionavyo ktk picha..
Hizi habari kila zinavyoendelea kutolewa zinanipa mashaka zaidi na Siasa au jinsi vyombo vyetu vya uchunguzi wa ajali vinavyofanya kazi. Ulimsikia OCD akisema ati lile shimo ndilo lilikuwa sababu wakati hajamhoji mtu hata mmoja wala kufuatilia lile lori limekwenda wapi na kwa nini waliondoka sehemu ya ajali!
 
Mkandara,

Jana niliambiwa na polisi mmoja kwamba dereva wa lori lililohusika na ajali alishahojiwa na polisi. Nashangaa sijaona mahali popote wakiandika. Nilimwuliza huyo jamaa kama anachosema ni kweli na alisema dereva amepatikana na alishahojiwa na polisi.

Labda watu kama Mpita Njia wanaweza kutusaidia kujua ukweli kwa kuongea na huyo mkuu wa polisi wa mkoa.

Ukiangalia polisi wenyewe mpaka waandishi wa habari unabaki kuishiwa nguvu maana ni kama wanakuja na statements mbalimbali bila uchunguzi wa maana. Wanakuwa kama sisi hapa JF ambao tunaweza kusema lolote. Vyombo vinavyotegemewa na wanachi vinatakiwa kuwa makini zaidi kwenye statements wanazotoa maana zinaweza kuwa na madhara kwenye jamii.

Labda watu wengi si maderva, lakini effect ya kugongwa kwa nyuma ni kubwa mno na naamini effect yake ingelikuwa hata kubwa zaidi.
 
FMES,



Kitu ambacho labda waandishi wetu pamoja na polisi wameshindwa kufanya uchunguzi, ni je ni kweli Mwakyembe alilala Makambako? Kama alilala makambako waliondoka hapo saa ngapi? Kutoka Makambako mpaka Ifunda kisheria ni masaa sio chini ya matatu, kama walifika Ifunda kwenye saa moja, kuna mawili, waliondoka mapema sana au walikuwa wanakimbia sana.

Pia inasemekana waliondoka Kyela saa mbili usiku; kutoka Kyela mpaka Makambako ni kama masaa matano kama unafuata sheria za barabarani. Sasa kama ni kweli ina maana walifika Makambako masaa ya saa saba, watafute guest na kulala na kuondoka kama saa kumi asubuhi, je ina make sense?

Kitu kingine ambacho inatakiwa kujua mnapochangia hili jambo ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake. Kwenye mikutano yake mingi hudiriki hata kusema kuna watu wamejaribu kumpa mamilioni huyo dereva ili amwue lakini dereva siku zote anakataa. Huwa najiuliza kama kuna hayo mambo kwanini hawaendi polisi? Labda ni maneno ya kisiasa zaidi kuliko ukweli. Kilicho ukweli ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake na ningetegemea kabisa afanye lolote lile kujaribu kumwokoa asiingie matatizoni.
Engineer punguza speculations usizokuwa na uhakika nazo.Zinapunguza reliability yako kwa mtu anayeita Engineer(proffession ya mambo hakika)
Kwa tarifa yako Makambako hadi Iringa kuna kilometa karibu 180, hata mabasi hayachukui masaa 3 kusafiri mwendo huo, sembuse gari dogo linaloenda 120km per hr!
 
Back
Top Bottom