Rutakyamilwa
JF-Expert Member
- Feb 27, 2009
- 1,871
- 1,237
thank god. Alikuwa amepata shock ya ajali na sasa amezinduka. Madaktari wametuondoa hofu kuwa hana majeraha makubwa. Wanasubiri vipimo kufanya uchunguzi zaidi kabla hawajamruhusu kutoka.
Hivi na wewe ukifa leo kwa bahati/bahati mbaya nani atajua?Wapinga ufisadi wote hawapaswi kupata ajali, kuugua, kuandikwa vibaya, kukosolewa,.... na ikitokea hayo mabalaa yakawakuta, mafisadi waandamwe, walaaniwe,...Hebu tukuekue kidogo WATANZANIA wenzangu.
Asante mkuu, nilikuwa najua ni kabla ya Iringa lakini sikuwa na uhakika ni mbali kiasi gani.Mtanzania hapo si karibu na jia panda ya mjini kwa kuna kilomita karibu 40 au zaidi mpaka kufika njia panda ya town
kutokana na jambo ili nimejifunza mambo mengi sana hapa.kumbe JF karibu member wote ni wacha Mungu kiasi hiki? mmh!
LATEST: Mpiganaji Dk Harrison Mwakyembe atapelekwa Dar kwa charter plane mchana huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kidaktari. Kwa sasa anaendelea vizuri Wadi No 5 katika hospitali ya mkoa Iringa. Dereva wake ni mzima kabisa, na yuko chini ya ulinzi wa polisi kwa sasa, hapo hapo hospitali. Anahojiwa kutokana na kudanganya hapo awali kuwa gari yake iligongwa kwa nyuma. Mtu aliyeenda eneo la ajali na baadaye hospitali anasema gari ya Dr Mwakyembe aina ya Landcruiser ilikuwa ina-overtake malori mawili na ghafla dereva alishtukia shimo kubwa mbele yake akapoteza control na gari ikapinduka ikiwa pia imegonga mti mkubwa na kuuong'oa.