Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

nsaji mpoki, tunakushukuru sana kwa kazi nzito uliyoifanya ya kutuhabarisha tangu asubuhi, umekuwa mtu wa faraja sana kwetu, naomba tuwaachie kijiti hicho watu walioko dsm ili waweze kutupa habari za huko.
 
JF mnafanya kazi nzuri,appreciated, Dr.Mwakyembe still God wants you for the purpose of our Nation, Imen.
 
Thanks all. We wish him all the best of luck and quick recovery.
 
Naamini atakuwa ameshapanda hiyo ndege na ninaamini zaidi kuwa ana uangalizi wa mtu wa karibu sana sana ndani ya ndege ya Serikali!!!! N jicho la ndugu yake huyo liwe halitizami sana pembeni, wala haitwi itwi aache mgonjwa ili kwenda kusikiliza jambo!!!! Kama ni discussion yoyote ifanyike akiwa close to our hero!!!
 
Pole Sana Dr. Mwakyembe.

Naamini vita dhidi ya ufisadi itaendelea. Hata kama ni mafisadi, hawatatumaliza wapiganaji sote.

Poleeeeeeeeeeeee!
 
Sawa kabisa Maane. Lazima tuhakikishe mpiganaji wetu anakuwa salama baada ya ku-survive kwenye hiyo accident mbaya. Mie nitapita pale MOI baada ya kazi kufuatilia hali yake. In the meantime, sala zetu wapiganaji wote ni muhimu ili Mungu amnusuru. Naamini Mola atasikiliza sala zetu kwani anajua jinsi tunavyomhitaji kamanda huyu katika mapambano makali yaliyoanza ya kuikomboa nchi yetu kutoka mikononi mwa mafisadi papa na vibaraka wao wengi waliopo serikalini. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Chanzo cha ajali ni nini........moja naweza kusema ile sehemu inahitaji umakini (sababu ya road undulations + potholes) mkubwa kwa dereva yeyote (hakuna cha uzoefu pale), pili uchovu wa dereva kama aliendesha muda mrefu, tatu yaweza kuwa malfunction kwenye gari lenyewe........

walioshuhudia ajali watueleze chanzo cha ajali......

BTW.......Pole sana Mheshimiwa.......nakutakia afya njema pamoja na wenzako mliokuwa kwenye hiyo ajali
 
Wakuu,
nimepata habari kuwa Dr. Mwakyembe amepata ajali huko Iringa. Kama kuna mwenye habari kamili atupatie maana nasikia haongei. Iringa mpo? Tuhabarisheni....
 
.......sipo Iringa lakini nimeambiwa pia, ameumia TAYA, lakini aliweza kuongea na anapelekwa dar.
 
Duniani kuna watu na viatu! did the world really need Hitler,Bokassa au Nduli Amin?

Chanzo cha ajali wanasema dereva alikuwa anajaribu kuovertake roli, akiwa kwenye mwendo mkali ghafla akakutana na shimo, tairi la mbele likachomoka wakaparamia mti! vibaka wakafanya sherehe... wa kuwaonea huruma ndo kuwakimbiza hospt.

Thanks God wanaendelea vyema.
 
Naamini atakuwa ameshapanda hiyo ndege na ninaamini zaidi kuwa ana uangalizi wa mtu wa karibu sana sana ndani ya ndege ya Serikali!!!! N jicho la ndugu yake huyo liwe halitizami sana pembeni, wala haitwi itwi aache mgonjwa ili kwenda kusikiliza jambo!!!! Kama ni discussion yoyote ifanyike akiwa close to our hero!!!

Msiwe na wasiwasi. Dr Mwakyembe ameruka kama dk. 15 hivi zilizopita kuelekea Dar. Nilikuwa Uwanja wa Ndege wa Iringa maarufu kama Nduli Airport. Ni mwendo wa saa 1.00 hivi kwa ndege kutoka Iringa kwenda Dar. Hivyo wana JF wa DSM mnaweza kupiga jicho pale airport wakitua. Kutoka huku amesindikizwa na Dr. aitwae Nyabusani ambaye tangu alipoingia hospitali alikuwa akimhudumia. Tuna imani atafika salama na atapona haraka.
 
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa afande Advocate Nyombi ajali hii imetokea pale gari ya Dr. Mwakyembe ilipokuwa inataka kulipita lori, ambapo gari hilo la mbunge likagonga shimo lililo katikati ya barabara. Baada ya kugonga shimo, gurudumu likachomoka na gari kumshinda dereva, likagonga mti na kupinduka vibaya.
Ajali hii imetokea eneo la Ifunda.


Nawatakia majeruhi afya njema na Mungu awajalie wapone na waendelee na majukumu ya kulijenga taifa.
gurudumu likachomoka? really? isijekuwa kuna mtu alilegeza nati za gurudumu kabla ya safari!!!!!
 
Pole , Mungu wetu ni mwema!

Wewe nawe, ustaarabu ni kitu cha bure.

Hajaropoka humu, wewe kinakuwashia nini. Rekebisha na jirekebishe haloo kabla haujavuliwa nguo na wewe.

gurudumu likachomoka? really? isijekuwa kuna mtu alilegeza nati za gurudumu kabla ya safari!!!!!

Barabara ile unaijua au unaisikia? kwanza nyembamba...pili kuna mashimo makubwa na madogo ya kushtukiza, tatu sehemu nyingi zimetitia hivyo ni kunesa utadhani uko kwenye bembea.
 
Inasemekana kuwa dereva wake alikuwa akiovateki (akilipita) lori, lakini kwa bahati mbaya akagonga kwenye shimo lililoko barabarani na kulifanya gari lipinduke mara kadhaa!
Naamini Mungu atamponya! AMEEEEEEEEEN!!!!!

Miezi michache iliyopita nilipita barabara hiyo. Kwa kweli kipande cha Mafinga-Iringa kilikuwa kibaya na matengenezo yalikuwa yanafanyika sehemu kadhaa.

Pole Dr. Mwakyembe.
 
gurudumu likachomoka? really? isijekuwa kuna mtu alilegeza nati za gurudumu kabla ya safari!!!!!

Yote yanawezekana mkuu, kwani hujasikia salamu za pole kutoka TBC? halafu wajameni, hivi hiyo TBC namna gani? hadi salamu za watu zinarushwa ama zimelipiwa? and what is special na hizo salamu why him?
 
Back
Top Bottom