Ajali ya gari Bagamoyo

Ajali ya gari Bagamoyo

hydroxo

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
3,553
Reaction score
7,334
Wakuu leo kumetokea ajali mbaya sana Bagamoyo.

Mwenye taarifa za uhakika kuhusu ajari hii atujuze.

===
Coaster inayofanya safari zake kutoka Bagamoyo kwenda Morogoro, imepata ajali kwa kugongana na Canter katika kijiji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo asubuhi ya January 8, 2023.

Watu watano wameripotiwa kufariki katika ajali hiyo na wengine 10 wakiwa katika hali mbaya na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.

Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo. Aidha watu waliokuwa na majeraha madogo wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao.
 
Watanzania wengi huwa ni wabishi kutii sheria za barabarani hasa mwendokasi. Ajali ikitokea ndio wa kwanza kusema ni Mipango ya Mungu.

Tutazidi kuangamia kwa huu ubishi hadi pale Akili zetu zitakapo kaa Sawasawa na kuchukua hatua kali kudhibiti ajali....
 
Pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao .. na pole pia kwa majeruhi Mwenyezi Mungu awaponye
 
Watanzania wanakufa kizembe

Wanakufa kama sisimizi

Ova
 
Back
Top Bottom